Home Mchanganyiko Katibu Mkuu: Kampeni ya marufuku ya mifuko ya plastiki inaenda vizuri

Katibu Mkuu: Kampeni ya marufuku ya mifuko ya plastiki inaenda vizuri

0

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (katikati)
akifafanua kuhusu vifungashio alipozungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani)jijini Dodoma. Wengine pichani kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine na Mkurugenzi Mkuu Baraza la Hifadhi
na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), dK. Samuel Gwamaka.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akionesha
baadhi ya viungashio vinavyotumika kwa matumizi ya kubebea bidhaa nyingine
tofauti na inayotakiwa.

Naibu Katibu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi Joseph Sokoine akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akionesha
mfuko mbadala unaoruhusiwa kubebea.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo akionesha
kifungashio kilichofungwa nyama bila kukidhi vigezo vinavyotwakiwa.

Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais
kufafanua nkuhusu vifungashio.

**************************

Serikali imesema kampeni ya kupiga marufuku mifuko ya plastiki inakwenda
vizuri na kusisitiza ni makosa kisheria kubadili matumizi ya vifungashio vya
bidhaa maalumu na kutumika kama mifuko ya kubebea bidhaa mbalimbali huku.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo amebainisha
hayo leo jijini Dodoma alipozungumzia azma ya Serikali ya kuendesha
operesheni maalumu nchi nzima ya uzingatiaji wa sheria ya usimamizi wa
mazingira juu ya marufuku ya mifuko ya plastiki na matumizi endelevu ya mifuko
mbadala.

Alisema adhabu stahiki zitatolewa kwa watengenezaji, waingizaji, wasambazaji
na watumiaji wa vifungashio vya plastiki vilivyozalishwa ama kuingizwa nchini na
kutumika kama vibebeo vya bidhaa.

"Baada ya kuanza kwa utekelezaji wa Katazo la Kutumia mifuko ya Plastiki
imebainika kuwa baadhi ya wazalishaji na wasambazaji wamebadilisha matumizi
ya mifuko laini ya plastiki isiyokuwa na mishikio na kuitumia kama vibebeo vya
bidhaa," alisema Mhandisi Malongo.

Alisema Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na kikosi kazi inaendelea na
zoezi la kuelimisha umma juu ya jambo hili pamoja na kuhamasisha matumizi ya
mifuko mbadala.

Kwa mujibu wa Kanuni za Usimamizi wa Mazingira za Kupiga Marufuku Mifuko
ya Plastiki za Mwaka 2019, ni marufuku kuzalisha, kuingiza nchini, kusambaza
na kutumia mifuko ya plastiki iliyotajwa katika Katazo hili.

Alisema Kanuni ya 9 inatoa msamaha kwa baadhi ya vifungashio vya plastiki
kwa ajili ya huduma za afya au ambavyo vinatumika kwenye kufungashia bidhaa
za viwandani, sekta ya ujenzi, sekta ya kilimo, vyakula au usafi na udhibiti wa
taka.
"Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linaanda viwango kwa vifungashio hivi
ambavyo vitalazimisha kiwango cha unene, uwekwaji lakiri na kutambulisha
bidhaa iliyofungashwa kabla ya kuuzwa," alisema.