NJOMBE
Tatizo la lishe kamili na lishe linganifu katika mazao limetajwa kuwa sababu ya kupungua kwa uzalishaji kwa mazao mkoani Njombe na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima ambao wamekuwa wakutumia gharama kubwa katika maandalishi ya shamba hadi mavuno.
Kufuatia changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na kampuni ya YARA imelazimika kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa ugani mkoani humo juu ya matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo pamoja na njia sahihi ya kukabillina na changamoto ya ongezeko la tundikali katika udongo ambayo imesababisha kupotea kwa rutuba na afya ya udongo rafiki kwa mazao.
Awali akifungua mafunzo kwa niaba ya katibu tawala mkoa wa Njombe Dr George Katemba ambaye ni afisa mifuko anaesimamia kitengo cha biashara,uchumi na mifugo pamoja Maurid Mkima bwanashamba mwandamizi kutoka kampuni hiyo wanasema elimu inatolewa kwa wataalamu hao ikasaidie kumaliza tatizo hilo linalowakabili wakulima wengi mkoani humo.
Nao baadhi ya maafisa ugani hao akiwemo Angela Mlowe watalaamu wengiwa kilimo wamekuwa na uelewa mdogo juu ya matumizi ya bora pembejeo jambo ambalo limekuwa likiwapa kigugumizi kutoa ushauri kwa wakulima na kueleza jinsi mafunzo yalivyowahimarisha.