******************
NA EMMANUEL MBATILO
Luis Enrique amejiuzulu nafasi ya ukocha mkuu wa timu ya taifa ya Hispania. Enrique hajamudu kumaliza walau mwaka mmoja katika nafasi hiyo.
Ikimbukwe kocha huyo aliachana na klabu ya Barcelona na kuamua kujiunga na Timu ya Taifa ya Spain baada ya kombe la Dunia hapo mwaka jana.
Zipo taarifa za chini chini kwamba anahitajika kunako klabu ya Chelsea ambayo inahaha kutafuta kocha ambaye anaweza kuiongoza klabu hiyo kwa msimu ujao baada ya kuondoka kwa Maurizzio Sarri.