Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa akifurahia jambo wakati akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Shule za Sekondari kwa Ukanda wa Afrika Mashariki (FEASA) bwana Kariuki Gikonyo mara baada ya Mkuu wa mkoa kugawa medali za dhahabu kwa washiriki wanne wa riadha maalum leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara.
Washindi wa kwanza hadi wa tatu kutoka mikoa ya Pwani, Unguja na Njombe wakisubiri kupewa medali zao za dhahabu, fedha na shaba leo katika viwanja vya chuo cha ualimu Mtwara
Mjumbe wa kamati ya usimamizi UMISSETA taifa kutoka Wizara ya Elimu Salum Salum (mwenye tracksuit ya kijani) akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa riadha maalum na makocha wao mara baada ya kuwakabidhi medali zao
………………
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Mikoa ya Pwani, Simiyu, na Singida ndiyo inayoonekana kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya UMISSETA yanayotarajiwa kukamilika tarehe 21 juni 2019.
Mkoa wa Pwani umepata medali 7 za dhahabu, 1 ya fedha na 2 za shaba, na hivyo kujipatia jumla ya medali 10 kwenye mashindano hayo.
Simiyu imepata medali 2 za dhahabu, 5 za fedha na 2 za shaba jumla ina medali 9
Mkoa wa Singida nao haukuwa nyuma katika kupata medali ambapo walipata medali 3 za dhahabu, 5 za fedha na 3 za shaba, hivyo jumla wamepata medali 11.
Mkoa wa Mwanza nao haukuwa nyuma katika kupata medali ambapo walifanikiwa kupata medali 3 za dhahabu, huku jirani zao shinyanga wakipa media 1 ya dhahabu, 1 ya fedha na 2 za shaba.
Mkoa wa Geita nao ulipata media 1 ya dhahabu, wakati Tabora wao walipata media 1 ya dhahabu, 3 za fedha na 1 ya shaba, na Manyara wamepata medali 2 za fedha na 5 za shaba, huku wenzao wa Arusha wamepata medali 2 za dhahabu 1 ya fedha.
Mkoa wa Unguja nao haukuwa nyuma katika ushindi wa medali mwaka huu ambapo walijinyakulia medali 3 za dhahabu, 1 ya fedha na 1 ya shaba.
Mikoa mingine ambayo haikutoka kapa ni pamoja na Dar es salaam ambao wamepata medali 3 za dhahabu, 1 ya fedha na 1 ya shaba, mkosa wa Lindi nao ulipata medali moja ya fedha huku mikoa mingine 11 ikiambulia patupu.
Mikoa iliyokosa kabisa medali katika mashindano ya riadha mwaka huu ni pamoja na Katavi, Ruvuma, Tanga, Pemba, Mtwara, Njombe, na Rukwa.
Mikoa mingine ni pamoja na Iringa, Kagera Songwe na Morogoro.