****************************
NJOMBE
Naibu katibu mkuu wa wizara ya maji mhandisi Emmanuel Kalombelo amemuagiza katibu tawala wa mkoa wa Njombe na mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Njombe kumpoka nafasi ya ukuu wa idara mhandisi wa maji wa halmashauri hiyo Bakari Kitogota kwa madai ya kwamba mtalaamu huyo ameshindwa kutekeleza majukumui yake hatua ambayo imesababisha mradi wa maji wa Lugenge kuchelewa kukamilika licha ya Maji kufika kwenye tenki kuu.
Mhandisi Katobelo ametoa agizo hilo baada ya kutembelea na kukagua mradi huo ambao una miaka zaidi ya mitano tangu uanze kutekelezwa bila ya kukamilika huku ukiwa umetumia mabilioni ya fedha hadi sasa .
Mbali na kuchelewa kukamilika kwake naibu katibu mkuu wa wizara ya maji Kitobelo ameonyeshwa kukasirishwa na kitendo cha maji kufika katika matenki na kuishia kumwagika bila sababu za msingi huku akidai kwamba kutokana na uzembe huo mhandisi huyo wa maji wa amekuwa akikwepa kushiriki kwenye ziara yake kwani anatambua makosa yake.
Akifafanua hatua atakazochukua dhidi ya watumishi wazembe katika kikao cha tathimini ya ziara hiyo mara baada ya kuambiwa changamoto hiyo katibu tawala wa mkoa wa Njombe Charles Kichele anatoa onyo kwa watumishi wazembe kwamba atawachukulia hatua kali za kisheria kwa watumishi wa umma.
Kwa upande wao wakazi wa mijiji cha Lugenge akiwemo Kandidus Msema wanasema watalaamu wanaotekeleza mradi huo wamekuwa wakichangamka pindi wanapo sikia ujio wa kiongozi mkubwa wa serikali na kueleza jinsi wanavyo athirika kwa kufata maji mabondeni kwa sasa.