Home Mchanganyiko JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA WATANO (5) AMBAO WANAHUSISHWA...

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA WATANO (5) AMBAO WANAHUSISHWA NA MAKOSA MBALIMBALI

0

************************

TUKIO LA KWANZA;-

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA WAKATI LINAENDELEA NA
HARAKATI ZA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA LIMEFANIKIWA
KUKAMATA WATUHUMIWA WAWILI (2) KWA KOSA LA KUSAFIRISHA
DAWA ZA KULEVYA AINA YA BHANGI KIASI CHA MAGUNIA NNE (4)
YENYE UZITO WA KILOGRAMU 520, TOKA IBAMBO – MKOANI
TABORA KUJA MWANZA, HUKO ENEO LA NYAMAZOBE WILAYANI
NYAMAGANA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 14.06.2019 MAJIRA YA 22:15HRS,
HII NI BAADA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KUPATA
TAARIFA ZA KIINTELEJENSIA KWAMBA ENEO TAJWA HAPO JUU
KUNA GARI LIMESHUSHA MAGUNIA MANNE YA BHANGI KISHA
LIMEONDOKA ENEO LA TUKIO.

POLISI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO
NA KUWAFANIKIWA KUKAMATA WATUHUMIWA WA WAWILI AMBAO
NI;-1. KASENZA MATHIAS, MIAKA 39, MSUKUMA, MKAZI WA IBAMBO –
TABORA NA 2. LEMBO BUHENDELA, MIAKA 29, MSUKUMA, IBAMBO
–TABORA, WAKIWA NA MAGUNIA MANNE YA BHANGI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA NA MAHOJIANO
NA WATUHUMIWA WAWILI ILI KUWEZA KUBAINI MTANDAO MZIMA
WA KUSAFIRISHA DAWA HIZO ZA KULEVYA. SAMBAMBA NA HILO

MSAKO WA KULISAKA GARI LILILOSAFIRISHA BHANGI HIZO BADO
UNAENDELEA.

TUKIO LA PILI;
MTU MMOJA AITWAYE FUNGO MAYALA, MIAKA 34, MSUKUMA,
MFANYABIASHARA WA SAMAKI, MKAZI WA MHANDU – KISIWANI
AMEMSHAMBULIA KWA KUMPIGA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI
WAKE NA KUMKABA SHINGO HADI KUFA HAMIDA JOSEPH, MIAKA
30, MUHA, MJASILIAMALI, MKAZI WA MHANDU – KISIWANI,
BAADAYE KUJITEKETEZA KWA MOTO, HUKO MHANDU KISIWANI
WILAYA YA NYAMAGANA, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 18.06.2019 MAJIRA YA 16:00HRS,
BAADA YA MGOGORO WA KIMAPENZI WA MUDA MREFU KATI YA
MAREHEMU NA MTUHUMIWA AMBAPO MAREHEMU ALIMRIPOTI
MTUHUMIWA POLISI, KISHA ASKARI WALIMKAMATA MTUHUMIWA NA
KUMFIKISHA MAHAKAMANI TAREHE 11/06/2019.

HATA HIVYO, TAREHE 18/06/2019 SIKU AMBAYO KESI ILIPANGWA
KUSIKILIZWA MAREHEMU ALIKWENDA MAHAKANI KUOMBA
KUMSAMEHE MSHITAKIWA HUYO, MAHAKAMA ILIRIDHIA OMBI HILO
NA KUONDOA KESI HIYO MAHAKAMANI.

AIDHA BAADA YA MSAMAHA HUO MTUHUMIWA ALIKWENDA
NYUMBANI KWA MAREHEMU NA KUINGIA NDANI KISHA ALIFUNGA
MLANGO NA KUANZA KUMPIGA MAREHMU NDIPO MAJIRANI
WALISIKIA KELELE ZA MAREHEMU AKIOMBA MSAADA LAKINI
WALISHINDWA KUFUNGUA MLANGO NDIPO WALITOA TAARIFA
POLISI.

POLISI WALIFIKA KWA HARAKA ENEO LA TUKIO NA KUKUTA
NYUMBA YOTE IKIWA INAFUKA MOSHI NA KUSHIRIKIANA NA
MAJIRANI KUVUNJA MLANGO, NDIPO WALIMKUTA MAREHEMU
AKIWA TAYARI AMEFARIKI DUNIA HUKU MOTO UKIWA
UMEMUUNGUZA SEHEMU MBALIMBALI YA MWILI WAKE.

VILEVILE MTUHUMIWA ALIKUTWA AKIWA MAHUTUTI KUTOKANA NA
MAJERAHA YA MOTO NA KUKOSA HEWA KUTOKANA NA MOSHI,
POLISI WALIMCHUKUA NA KUMPELEKA HOSPITALI LAKINI ALIFARIKI
DUNIA WAKIWA NJIANI. MIILI YA MAREHEMU WOTE WAWILI
IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MKOA SEKOU TOURE KWA AJALI YA
UCHUNGUZI WA DAKTARI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA
ITAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

TUKIO LA TATU;
MTU MMOJA MWANAUME AITWAYE SHIGANGA LUHEKE, MIAKA 38,
MKULIMA, MKAZI WA MTALE, AMEUWAWA NA KUNDI LA WATU
WALIOTENDA KINYUME NA SHERIA BAADA YA KUKAMATWA NA
KUKU WAWILI WA WIZI, HUKO KIJIJI CHA ITANDULA, KATA YA
LUTALE, WILAYA YA MAGU.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 17.06.2019 MAJIRA YA 00:30HRS,
HII NI BAADA YA MAREHEMU KUKAMATWA NA WANANCHI AKIWA NA
KUKU WAWILI AMBAO INADAIWA KUWA AMEWAIBA, NDIPO
WALIMSHAMBULIA KWA KUMPIGA KWA MAWE NA FIMBO SEHEMU
MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA KUPELEKEA MAREHEMU
KUPOTEZA MAISHA PAPO HAPO.

AIDHA, JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAMSHIKILIWA
MWENYEKITI WA KITONGOJI HICHO KUTOKANA NA KUHUSIKA KWA
NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA MAUAJI HAYO, AIDHA MSAKO
WA KUWATAFUTA WATU WENGINE AMBAO WANADAIWA KUHUSIKA
KATIKA MAAUJI HAYO BADO UNAENDELEA.

TUKIO LA NNE;
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI
AMBAO NI MARIAM JOSEPH, MIAKA 21, MSUKUMA, MKAZI WA
TARIME NA JENIPHA MWITA, MIAKA 25, MKURYA, MKAZI WA TARIME,
KWA KOSA LA KUPATIKANA NA DAWA ZA KULEVYA AINA YA
MIRUNGI KIASI CHA KILOGRAMU SITA (6), HUKO KWENYE KIZUIZI CHA MAGARI TRA, WILAYA YA MAGU, KITENDO AMBACHO NI KOSA
KISHERIA.

TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 16.06.2019 MAJIRA YA 13:00HRS,
HII NI BAADA ASKARI KUTILIA SHAKA BASI LA KAMPUNI YA ZAKARIA
LENYE NAMBA T. 270 DAN ITOKAYO TARIME KUJA MWANZA, NDIPO
WALILISIMAMISHA NA KULIFANYIA UPEKUZI NA KUWAKAMATA
WANAWAKE HAO WAWILI WAKIWA NA DAWA HIZO ZA KULEVYA
AINA YA MIRUNGI KIASI CHA KILOGRAMU TATU (3), KILA MMOJA
WAKIWA WAMEJIFUNGA KWENYE MIILI YAO.
TUKIO LA TANO,

MTU MMOJA AITWAYE JOSHUA STEVEN @ MOMGE, MIAKA 40,
MGANGA MKUU WILAYA YA UKEREWE, AMEFARIKI DUNIA BAADA YA
GARI ALILOKUA AKIENDESHA LENYE NAMBA T.4101 CAW AINA YA
TOYOTA IPSUM KUGONGA MTEMBEA KWA MIGUU AITWAYE
ATHUMAN NANDOYA, MIAKA 45, MFANYABIASHARA NA MKAZI WA
MTAA WA NYAMANORO, KISHA KUINGIA MTARONI, HUKO KATIKA
BARABARA YA MAKONGORO, MAENEO YA NYAMANORO WILAYANI
ILEMELA.

AJALI HIYO IMETOKEA TAREHE 16.06.2019 MAJIRA YA 05:00HRS
ALFAJIRI, MAJERUHI AMEKIMBIZWA HOSPITALI YA MKOA SEKOU
TOURE KUPATIWA MATIBABU, HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA BUGANDO
KWA AJILI YA UCHUNGUZI, CHANZO CHA AJARI BADO
KINACHUNGUZWA IKIWA NI PAMOJA NA KUWATUMIA WAKAGUZI WA
MAGARI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA ONYO KWA BAADHI
YA WANANCHI WENYE KUTENDA UHALIFU KUWA
WAACHE KWANI NI KINYUME NA SHERIA NA ENDAPO MTU/WATU
WATABAINIKA HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI
YAO. VILEVILE LINAWAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA
USHIRIKIANO KWA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU NA WAHALIFU
MAPEMA ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE
VYOMBO VYA SHERIA.