Injinia wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Ziwa Nyasa Bw. Hamis Nyemboakizungumza na waandishi wa habari wakati akielezea mradi wa maboresho ya Bandari ya Ndumbi wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.
……………………………………………………………
Bw. Richard Mahundi mmiliki wa mgodi wa Makaa ya Mawe (Liweta Coal Mining) ulioko kijiji cha Liweta Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kufanikisha usafiri wa mizigo katika ziwa Nyasa kufuatia ununuzi wa Meli mbili za mizigo MV Njombe na MV Ruvuma.
Mahundi ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ziara katika mgodi wake uliopo kijiji cha la Liweta, ambao sasa umeanza uzalishaji mara baada ya kukaa miaka 19 bila kufanya shughuli za uchimbaji kwa sababu ya changamoto ya kusafirishaji wa shehena ya makaa hayo ya mawe kutoka mgodini kwenda katika kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement mkoani Mbeya kupitia bandari ya Kiwira.
“Tulimiliki eneo hili toka mwaka 2000 lakini hatukuweza kuanza uzalishaji kutokana na changamoto ya Miundombinu iliyopo katika usafirishaji wa makaa hayo kwa sababu barabara bado mbovu lakini kwa sasa inaenda kuondolewa na usafiri wa meli hizo.
“Kwa sasa tunasafirisha tani 2,000 kwa mwezi lakini meli itaturahisishia kubeba walau tani 5,000 kwa wiki na mteja wetu mkubwa ni Kiwanda cha Saruji Mbeya (Mbeya Cement).
“Pamoja na hayo tunamuomba waziri mwenye dhamana atuangalie kwa jicho la tatu wachimbaji wazawa kwa sababu wazawa bado hatujapewa nafasi sana kama Rais Magufuli alivyodhamiria kuwainua wachimbaji wadogo wazawa,” alisema Mahundi.
Ameongeza kuwa wanazo oda za kutosha kutoka kiwanda cha Saruji cha Mbeya Cement ili kuwapelekea makaa ya mawe, Pia wako mbioni kupata oda zingine kutoka nchi ya Malawi hivyo kazi nzuri itafanyika kutokana na hali ya usafiri kuwa bora kwa sasa.
Naye Injinia wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Ziwa Nyasa Bw. Khamis Nyembo amesema tayari wameshaanza kujenga gati kubwa zaidi lenye urefu wa mita 100 katika bandari ya Ndumbi, Jengo la Ofisi, Sakafu Ngumu kwa ajili ya kuhifadhia Makaa ya Mawe na mizani kwa ajili ya maroli kupima uzito wa mzigo.
Ameongeza kuwa meli hizo zikianza kazi zitafanya safari nne kwa wiki jambalo litarahisisha usafiri wa makaa ya mawe kutoka Bandari ya Ndumbi hadi Kiwira.
Amewasihi wafanyabiashara kutumia Meli za MV Njombe na MV Ruvuma kwa ajili ya kusafirishia mizigo yao kwakuwa ni salama na zinabeba mzigo mingi kwa wakati mmoja.
Injinia wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Ziwa Nyasa Bw. Khamis Nyembo akionesha mizani iliyofungwa katika bandari ya Ndumbi tayari kwa ajili ya maroli kupima uzito wa Makaa ya Mawe.
Ujenzi wa Gati la Bandari ya Ndumbi ukiendelea.
Bw. Richard Mahundi mmiliki wa mgodi wa Makaa ya Mawe Liweta Coal Mining ulioko eneo la Liweta Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma akiwaelezea waandishi wa habari namna makaa ya mawe yanavyochimbwa.
Eneo la uchimbaji wa makaa ya mawe likitayarishwa kwa ajili ya kuchimba.
Baadhi ya Mashine zinazotumika katika uchimbaji wa makaa hayo.
Bw. Richard Mahundi mmiliki wa mgodi wa Makaa ya Mawe Liweta Coal Mining ulioko eneo la Liweta Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma akionyesha miamba ya Makaa ya Mawe yanayofaa na yasiyofaa.
Bw. Richard Mahundi mmiliki wa mgodi wa Makaa ya Mawe Liweta Coal Mining ulioko eneo la Liweta Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma akielezea ubora wa makaa ya mawe yanayopatikana katika mgodi wa Liweta ambayo yanafikia CV 6000 kwa viwango vya makaa hayo.
Makaa ya mawe yaliyochimbwa na kuhifadhiwa tayari kwa kusafirishwa.
Bw. Richard Mahundi mmiliki wa mgodi wa Makaa ya Mawe Liweta Coal Mining ulioko eneo la Liweta Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma akionesha Makaa ya Mawe yaliyotayari kwa kusafirishwa.
Baadhi ya picha mbalimbali zikionyesha eneo la mgodi wa Makaa ya Mawe wa Liweta Coal Mining ulioko wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.