Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Prof.Tadeo Satta akitoa maelezo kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( katikati) kuhusu ramani ya majengo ya tawi jipya la chuo hicho wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo Juni 17, 2019 kijiji cha Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFMkinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Prof. Prof.Tadeo Satta akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akifurahia jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Prof. Tadeo Satta wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi Wilayani Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sapiwi Wilayani Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi wakishuhudia zoezi la uchimbaji msingi wa baadhi ya majengo ya Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kinachojengwa Kata ya Sapiwi wialayni bariadi mkoani Simiyu, wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo Juni 17, 2019.
……………………..
Na Stella Kalinga, Simiyu
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof. Tadeo Satta amewahakikisha wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kuwa ujenzi wa awali wa tawi la Chuo hicho mkoani Simiyu ,unatarajia kukamilika mwezi Septemba mwaka huu na kuanza kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo 2019/2020 .
Profesa Satta ameyasema hayo Juni 17, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Tawi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Simiyu katika kijiji cha Sapiwi wilaya ya Bariadi.
Profesa Satta amesema kujengwa kwa kituo hicho kipya cha mafunzo kutachangia kuongeza udahili na kubainisha kuwa katika mpango mkakati wa chuo mwaka 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021, chuo kimejipanga kuongeza kutoa mafunzo kwa wateja wake hasa katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Simiyu inayotarajiwa kuchukua mikoa ya kanda ya ziwa mpaka Tabora.
Ameongeza kuwa azma ya chuo ni kuanza kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo 2019/2020 kuanzia ngazi ya cheti na matarajio ni kuhamisha wanafunzi wa ngazi ya cheti na stashahada kutoka Mwanza kuja Simiyu ili Mwanza zibaki kozi za jioni wanazosoma watu wanaotoka kazini.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amempongeza Makamu Mkuu wa Chuo IFM, Prof. Tadeo Satta kwa kuwa mtendaji wa mipango aliyoipanga na kutimiza ahadi ya kuanza kujenga tawi hilo mwaka huu, huku akitoa wito kwa wananchi wote kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hosteli, migahawa na nyumba za kupangisha watumishi.
“Tawi la Chuo cha IFM linajengwa Sapiwi watu wote wanaalikwa kuchangamkia fursa na wachangamikiaji wa fursa wa kwanza ni wana Sapiwi wenyewe, tungehitaji kupata hosteli, migahawa ya chakula, maeneo ya watu kunywa vinywaji na tutawaambia TANROADS waone namna ya kuweka “stendi” maana hapa Sapiwi kitakuwa kituo kikubwa” alisisitiza Mtaka.
Aidha, Mtaka amewahakikishia viongozi wa Chuo cha IFM kuwa viongozi wa Mkoa wataendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha azma ya kukamilisha ujenzi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwezesha mkandarasi kufanya kazi saa 24 kwa kuhakikisha kuna ulinzi na miundombinu ya umeme inakuwepo katika eneo la ujenzi.
Naye Mayunga Juma Mkazi wa kijiji cha Sapiwi amesema wananchi wa Sapiwi wanashukuru uwepo wa ujenzi huo kwani umesaidia kutoa ajira na kuwawezesha kupata fedha za kujikimu kimaisha.
Kwa upande wake Msimamizi wa Ujenzi huo kutoka Chuo cha Mafunzo ya Ufundi (VETA) Kagera, Baluye Mitinje ameahidi kusimamia na kuhakikisha ujenzi unafanyika usiku na mchana ili ukamilike kwa wakati.
Ujenzi wa awali wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha Tawi la Sapiwi utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia tisa na sabini na moja .