Home Mchanganyiko WAKULIMA MIHAMBWE WATAKIWA KUTAZAMA MAZAO MENGINE

WAKULIMA MIHAMBWE WATAKIWA KUTAZAMA MAZAO MENGINE

0

Na Mwandishi wetu Mihambwe

Wakulima wameshauliwa kutokutazama wala kutumainia aina moja ya Kilimo na badala yake watazame na kulima mazao mengineyo kwa ajili ya chakula na biashara pia.

Hayo yamebainishwa Leo Juni 17, 2019 na Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu alipokuwa akizungumza na Wakazi wa kijiji cha Namedi kilichopo kata ya Miuta ambapo amewasihi Wakulima wote ndani ya Tarafa ya Mihambwe kutokutegemea kilimo kimoja cha Korosho tu na badala yake watazame na mazao mengineyo kama vile Mtama, ufuta, Mpunga, alizeti, njugu kwa ajili ya biashara na chakula.

“Tusishupalie zao moja pekee la Korosho, fursa za mazao ya Kilimo kama vile Ufuta, Alizeti, Mpunga, Mihogo na mengineyo bado ipo na masoko yapo pia. Mathalani hivi sasa Ufuta unapokelewa Maghalani na bei ya kwenye minada ni takribani Tsh. 3000 kwa kilo. Au zao la Mihogo lina soko kubwa ndani na nje ya nchi. Wakazi Tarafa ya Mihambwe tupanue fikra zetu kwenye Kilimo kwani fursa ni nyingi.” Alisema Gavana Shilatu.

Katika mkutano huo Gavana Shilatu pia alisikiliza na kutatua kero za Wananchi kijijini hapo Namedi.

Mkutano huo ulihudhuliwa na Watendaji wa Vijiji kata ya Miuta pamoja na Afisa Maendeleo kata ya Miuta.