******************************************
NJOMBE
Ikiwa mwezi mmoja umepita tangu waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo kuzitaja halmashauri 23 nchini ambazo zimefanya vibaya katika utoaji wa mikopo ya vijana, wanawake na walemavu ikiwemo ya wilaya ya Njombe , hatimae halmashauri hiyo imetoa mikopo yenye thamani ya mil 194 kwa vikundi 86.
Kwa mujibu wa taarifa Jafo iliagiza ifikapo julai 20 kila halmashauri iwe imemaliza kutoka mikopo hiyo ambayo ipo kisheria huku ikitoaa onyo kwa atakae puuza hilo.
Kutokana na Agizo hilo imeichukua muda mfupi kuandaa fedha hiyo na kuitoa kwa vikundi vya wajasiriamali wilayani Njombe ambapo katika zoezi la kukabidhi hindi za mikopo hiyo mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kutimia kukuza biashara zao ili baadae waweze kutoa nafasi kwa watu wengine kusaidiwa.
Awali akizungumza mkuu huyo wa wilaya amewataka wanufaika wa mikopo hiyo pia kuwa waaminifu kwa kurejesha katika muda uliopangwa huku akidai kuwa mikopo ya walemavu imegawanyika katika mfumo wa utoaji ambapo unatolewa kwa mlemavu mwenyewe au kwa mlezi wake na kutoa onyo kwa walezi kutumia udhaifu wa walemavu kuwazulumu haki zao
Nae mkurugenzi wa halmashauri Ally Juma pamoja na mwenyekiti wa halmashauri Valentino Hongoli wanatumia fursa hiyo wanasema kiwango kilichotoilewa hadi sasa kimeifanya halmashauri hiyo kuvuka lengo kutoka asilimia mia moja hadi kufikia asilimia mia moja therathini na tano jambo ambalo ni neema kwa wajasiriamali wilayani Njombe.
Kwa upande wao wanufaika wa mikopo hiyo akiwemo Vitus Jonas ambaye ni mlemavu na Stela Ngongolo .wanaishukuru serikali kwa kutuwapa mikopo hiyo ili kuinua biashara huku pia wakisema kiwango cha asilimia 2 kati 10 kinachotolewa kwa walemavu ni kidogo hivyo serikali ione ulazima wa kuongeza.