****************************************
Dar es salaam, 18/06/2019
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, amewataka Maofisa na askari
kuhakikisha wanaendelea kutimiza wajibu wao kikamilifu na kutokujiingiza
kwenye masuala ya uhalifu ikiwemo kushiriki kwenye wizi wa dhahabu
sambamba na uhujum uchumi.
IGP Sirro, ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa
akizungumza na Maofisa na Wakaguzi wa Jeshi hilo ambapo amesema
kuwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa askari anayeshiriki kwenye
uhalifu ikiwemo kufukuzwa kazi pamojana kufikishwa mahakamani.
Hata hivyo IGP Sirro amesema Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu katika
kuhakikisha suala la uchaguzi linafanyika kwa amani na utulivu na kwamba
amewahakikishia wananchi usalama wao na mali zao na kuwataka
wananchi kuendelea kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa sahihi za
uhalifu na wahalifu.
Kwa upande wake kamishna wa kamisheni ya ushirikishwaji wa jamii CP
Mussa Ali Mussa, amesema kuwa, uhusiano kati ya jeshi la polisi na jamii
umeendelea kuimarika nchini kutokanana taarifa zinazoendelea kutolewa
kutoka kwa raia wema na wapenda amani.