Mmoja wa Wakufunzi wakijaribu kuelekeza ni namna gani wanaweza kutoa elimu hiyo kwa wafanyabiashara ambao pia waliweza kuhudhulia mkutano huo
Baadhi ya wafanyabiashara na Wanafunzi waliweza kuhudhulia mkutano huo katika Hoteli ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
*********************
Kwa mara ya kwanza nchini wafanyabiashara wameweza kukusanyika na kupata mafunzo katika Ukuaji wa Uchumi mafunzo yaliyoandaliwa na Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam wakiwemo wakufunzi kutoka katika sehemu mbalimbali wakishirikiana na wakufunzi wa Tanzania.
Ameyasema hayo leo Meneja wa Mawasiliano ya kibiashara wa Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam Bi. Lilian Kisasa baada ya kukaa kikao hicho kilichopewa jina la Commerce At it’s Best Event ambapo wakufunzi walieleza ni jinsi gani wanaweza kutoa mafunzo hayo kwa wafanyabiashara.
“lengo la mkutano huu ni kuwekeza hasa katika kubadilisha mtazamo katika ukuaji wa Uchumi, biashara na hali ya kidigitali inayoendelea”. Amesema Bi. Lilian.
Amesema wameangalia pia kwa wawekezaji zaidi hasa wamiliki wa biashara ambao katika mkutano huo waliweza kuhudhulia kwa kiwango kikubwa pamoja na wanafunzi ambao wanatoka katika vyuo mbalimbali.
“Hili wazo lilitolewa baada ya sisi kuona kuna gep katika ukuaji wa kidigitali na wafanyabiashara hasahasa katika upande wa mitandao ya kijamii”. Ameongeza Bi. Lilian