Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto lililojengwa katika Zahanati ya Matale, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu chini ya mradi wa RMNCH- UNFPA
Mratibu wa Mradi wa Afya ya Uzazi na Mtoto RMNCH-UNFPA na Huduma za Uuguzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi. Dinah Atinda akikagua Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto lililojengwa katika Zahanati ya Matale, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu chini ya mradi wa RMNCH- UNFPA
Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto lililojengwa katika Zahanati ya Matale, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu chini ya mradi wa RMNCH- UNFPA
Mratibu wa Mradi wa Afya ya Uzazi na Mtoto RMNCH-UNFPA na Huduma za Uuguzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi. Dinah Atinda akikagua Jengo la Wodi ya Mama na Mtoto lililojengwa katika Zahanati ya Matale, Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu chini ya mradi wa RMNCH- UNFPA
……………….
Na.Angela Msimbira SIMIYU
Timu ya ufuatiliaji inayoshughulika na Mradi wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa OR-TAMISEMI imekerwa na kusuasua kwa ujenzi wa Zahanati ya Matale, katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu .
Akiongea kwa niaba ya Timu hiyo Mratibu wa Mradi wa Afya ya Uzazi na Mtoto RMNCH-UNFPA na Huduma za Uuguzi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bi. Dinah Atinda amesema ujenzi wa zahanati hiyo umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu kutokana na baadhi ya vitu vingi kutokamilika na jengo hilo kutotumika licha ya kutakiwa kuanza kutoa huduma za mama na mtoto katika jengo hilo.
Ameyataja maeneo ambayo hayajakamilika kuwa ni uwekaji wa milango, ufungaji wa gata za kuvunia maji, uwekaji wa madirisha ya alluminium, uwekaji wa mfumo wa umeme, uwekaji wa marumaru upande wa vyooni , uchimbaji na ujenzi wa mashimo ya maji taka, uwekaji wa masinki wakati fedha zote zilitolewa kwa ajili ya ujenzi ambapo ujenzi huo ulikuwa unatakiwa kukamilika juni, 2018
“Ni jambo la kushangaza kuona Zahanati iliyotakiwa kuanza kutumika tangu 2018 mpaka leo haijaanza kufanya kazi japokuwa Serikali imeweza kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi huo, suala hili halipendezi na linarudisha nyuma maendeleo kwa jamii” amesisitiza Bi. Atinda
Amesema kuwa timu imegundua kuwa kuna matumizi ya fedha yasiyofuata miongozo yaliyofanywa wakati wa ujenzi wa miundombinu ya Zahanati hiyo ambapo taarifa zinaonyesha kuwa Fundi wa ujenzi amelipwa zaidi ya shilingi milioni 5 kati ya shilingi milioni 6 alizotakiwa kulipwa wakati sehemu kubwa ya ujenzi huo haujakamilika.
Bi. Atinda ameiagiza Timu za Usimamizi wa Huduma za Afya katika Mkoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ukamilishaji wa jengo hilo na kuanza kutumika ifikapo tarehe 30 juni, 2019 na kutumia fedha zilizopelekwa na TAMISEMI katika robo ya nne ya mwaka 2018/2019 kufanya usimamizi wa vituo vyote vya kutolea huduma za afya 38 vilivyofanyiwa maboresho chini ya mradi wa RMNCH- UNFPA na kuhakikisha vituo vyote vinaanza kutoa huduma kwa jamii.
Bi. Atinda amesema kuwa tathimini ya matumizi ya fedha iliyofanywa na mkaguzi wa ndani wa Halmashaiuri ya Mji wa Bariadi ifanyiwe kazi na kutolewa taarifa katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
Aidha Timu ya Ufuatiliaji kutoka OR-TAMISEMI ilifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi na matumizi ya Zahanati na Vituo vya afya vilivyojengwa Mkoani Simiyu chini ya mradi wa RMCH-UNFPA.