Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera akikagua tumbaku inayohaniwa kulanguliwa na (Vishada) Walanguzi.
……………………………………….
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera ameamrisha oparesheni kabambe ya masaa 48 Wilayani Mlele Mkoani humo kwa walanguzi wa Tumbaku maarufu (Vishada)
RC Homera ameamuru kukamatwa kwa Afisa ushirika wa wilaya kwa kutoa ushawishi kwa Mkuu wa Polisi OCD Kamugisha Wilaya ya Mlele kwamba awaachie watuhumiwa watatu walio shikwa na Marobota zaidi ya 400 katika nyumba zao kwa kigezo cha nyazifa zao na ukwasi wao wa fedha.
Afisa ushirika huyo Bwana Joseph Malima yuko mbaroni kwa mahojiano na Jeshi la Polisi na Takukuru na ameondolewa wilayani hapo kwa amri ya mkuu wa Mkoa huo RC Juma Homera
Waliokamatwa mpaka sasa ni Amos Luciana, Simon Kibiriti, Thadeo Peter,Justin S. Benjamin Malembeka ,Vicent Mwacha ,Patrin John Soka na Thadeus Mmasi.
Watuhumiwa ambao bado wanatafutwa na Jeshi la Polisi ni Nicholus John Soka, Masumbuko Kyogo na mtu aliyefahamika kwa jina moja la Mnisi.
Naye Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Rachael Kasanda ambaye anaongoza oparesheni hiyo amesema mpaka jana tarehe 15/06/2019 zaidi ya marobota 700 ya tumbaku yamekamatwa na iko tumbaku isiyofungwa na inakadiriwa kufikia marobota zaidi ya 800 ambayo inakadiriwa kuwa kuwa tani 50 mpaka 60 za Tumbaku zinazofikia tahamani kati ya shilingi za kitanzania Milioni 200 mpaka 250.
Aidha mkuu wa mkoa Mh. Juma Homera ametoa maagizo ya kuanza kwa oparesheni hiyo baada ya malalamiko ya wananchi kwamba tumbaku inanufaisha zaidi wafanyabiashara wa wachache wa Inyonga wilayani Mlele kuliko wananchi.
Tayari tumbaku daraja la kwanza yote ilinunuliwa na wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya Inyonga ambapo mpaka watumishi wa umma wamekuwa wakijihusisha na Biashara hiyo.
Tumbaku ikiwa katika matayarisho
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera akikagua marobota ya tumbaku inayodhaniwa kulanguliwa na (Vishada) Walanguzi wa Tumbaku.