Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Mh. Asid Mtanda akizungumza na waandishi wa habari katika Bandari Bubu ya Kirando ziwa Tanganyika wakati alipofanya ziara na Meneja wa Bandari (TPA) Kigoma ziwa Tanganyika Ajuaye Kheri Msese katika bandari bubu hiyo.
……………………………………………….
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Mh. Asid Mtanda amepiga marufuku wakazi wa mji wa Kirando kutumia eneo hilo kama Bandari bubu badala yake watumie bandari ya Kipili ambayo ina miuondombinu yote muhimu na usalama kwa vyombo vya majini kutokana na kina chake kuwa kirefu.
Mkuu wa wilaya huyo alipiga marufuku wakati alipofanya ukaguzi katika bandari bubu hiyo akiongozana na Meneja wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Kigoma Ziwa Tanganyika Bw. Ajuaye Kheri Msese pamoja na waandishi wa habari.
Mtanda amewataka wananchi wote wenye vyombo vya usafiri wa majini kutumia bandari ya kipiri kwa sababu maofisa wote wa idara za serikali wanapatikana pale sa siyo bandari bubu ya Kirando.
“Tutafanya msako kwa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari kuangalia bandari bubu zote ambazo hazijarasimishwa zifungwe ili bandari ya Kipiri iendelee kutumika kutoa huduma za usafiri wa majini kwakuwa ndiyo bandari pekee katika eneo hilo yenye miundombinu yote.
Serikali inahitaji kodi na lazima ikusanye kupitia bandari ya Kipili kwa ajili ya kudhibiti ukusanyaji wa mapato vizuri kuliko kutumia bandari bubu ambazo hazina maofisa, lakini pia siyo salama kama ilivyo Bandari hiyo.
Eneo lote la maji katika ziwa Tanganyika ni mipaka kwa sababu tunapakana na nchi za Burundi, Zambia na DRC Congo hivyo hata udhibiti na ukaguzi kwa wageni wanaoingia nchini unaweza kufanyika vizuri katika bandari ya Kipili hasa kutokana na mambo mbalimbali ya kiusalama ukiwemo ugonjwa wa Ebola ambao upo katika nchi jirani ya DRC Congo.
Naye Meneja wa Bandari (TPA) Kigoma ziwa Tanganyika Ajuaye Kheri Msese akiielezea bandari hiyo amesema imekamilika kwa silimia 100 na iko tayari kwa kutumika muhimu ni wananchi kuitumia bandari hii usafiri wa kwenda kokote waendako na kusafirisha mizigo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Mh. Asid Mtanda akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu shehena ya mahindi iliyokutwa imetelekezwa katika bandari bubu hiyo na watu wasiofahamika, baada ya kugundua Mkuu wa wilaya hiyo anatembelea eneo hilo, Shehena hiyo ilikuwa inasafirishwa kwenda DRC Congo kupitia bandari bubu ya Kirando.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Mh. Asid Mtanda akizungumza na mmoja wa wananchi aliyetaka kupata ufafanuzi kuhusu katazo hilo, hata hivyo alipopata maelezo alielewa na kukubaliana na uamuzi wa serikali kuzuia matumizi ya bandari hiyo isiyo rasmi.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Mh. Asid Mtanda akizungumza na Meneja wa Bandari (TPA) Kigoma ziwa Tanganyika Ajuaye Kheri Msese katika bandari bubu hiyo.
Meneja wa Bandari (TPA) Kigoma ziwa Tanganyika Ajuaye Kheri Msese akiwaelezea waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa bandari hiyo uliokamilika kwa asilimia 100.
Manjengo ya Abiria na kuhifadhia mizigo yaliyojengwa katika bandari ya Kipili.
Gati la Bandari ya Kipili linayoonekana kwa uelekeo wa kwenda ziwani.
Gati la Bandari ya Kipili linavyoonekana kwa juu kutokea ziwani.
Gati la Bandari ya Kipili linavyoonekana kwa juu