Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akisalimiana na wajumbe wa Baraza la Watoto Taifa katika uzinduzi wa Kitini cha Mafunzo ya uwezeshaji wa mabaraza ya watoto nchini uliofanyika mkoani Geita kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika Juni, 16 pembeni yake ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Joel Festo.
Katibu Mkuu Idara Kuu maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu (kushoto) akikata utepe kuashiri uzinduzi wa Kitini cha Mafunzo ya Uwezeshaji wa Mabaraza ya watoto nchini uliofanyika mkoani Geita kueleeka Siku ya Mtoto wa Afrika Juni, 16 wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la watoto la Taifa Joel Festo kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Save The Children Bi. Neema Bwaira na wa pili kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Geita Bw. Denis Bandisa.
Katibu Mkuu Idara Kuu maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akizungumza katika uzinduzi wa Kitini cha Mafunzo ya Uwezeshaji wa Mabaraza ya watoto nchini uliofanyika mkoani Geita kueleeka Siku ya Mtoto wa Afrika Juni, 16.
Katibu Mkuu Idara Kuu maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu akiwa na wadau wa masuala ya Watoto, Maafisa kutoka Ofisi ya Mkoa wa Geita na Wajumbe wa Baraza la Watoto taifa wakionesha Kitini cha Mafunzo ya uwezeshaji wa mabaraza ya watoto nchini katika kuyaimarisha mabaraza ya watoto katika uzinduzi wa Kitini hicho uliofanyika mkoani Geita kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika Juni, 16
Baadhi ya watoto na wadau wa maendeleo ya mtoto wakifuatiia uzinduzi wa Kitini cha Mafunzo ya Uwezeshaji wa Mabaraza ya watoto nchini uliofanyika mkoani Geita kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika Juni, 16.
*******************
Na Mwandishi Wetu-Geita.
Serikali kwa Kushirikiana na Shirika la Save the Childreni imezindua Kitini cha Mafunzo ya Mabaraza ya watoto kwa lengo la kuboresha uelewa wa wajumbe wa mabaraza hayo nchini kufahamu kuhusu ukatili, uzalendo, uongozi na uwezo wa kushiriki katika kutoa maamuzi na masuala ya stadi za maisha.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa Kitini cha Mafunzo kwa uwezeshaji wa Mabaraza ya Watoto nchini leo Mkoani Geita Katibu Mkuu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amesema kuwa Kitini hiki kitatumiwa na Maafisa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hapa nchini kujenga uelewa wa aina moja kwa watoto nchini kuhusu masuala ya ukatili.
Dkt. John Jingu ameongeza kuwa hapo awali mafunzo yalikuwa yanatolewa katika mabaraza hayo hayakuwa yanatosheleza na hayakuweza kuwafikia watoto wengi na hivyo kurudisha nyuma jitihada za Serikali za ushiriki wa watoto nchini.
Pamoja na uzinduzi wa Mwongozo huo wa mafunzo ya Mabaraza ya Watoto nchini Dkt.Jingu pia amesema kuwa Mwaka 2009 Serikali kwa kushirikiana na wadau ilifanya utafiti kuhusu hali ya Ukatili Nchini na kufanikiwa kubaini aina na ukubwa wa tatizo la ukatili hapa nchini uliofanikisha mikakati inayofaa katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto hapa nchini.
“Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru wadau wote waliofanikisha hili nawasihi muendelee kushirikiana na Sserikali katika kuhakikisha malengo ya Kitini hiki yanafanikiwa” Alisema Dkt.Jingu
Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Mtoto nchini Bi. Mwajuma Magwiza ameongeza kuwa kabla ya kukamilika kwa mwongozo huu maalum utakaotumika kujenga uwezo wa wajumbe wa mabaraza ya Watoto hakukuwa na mwongozo maalum uliotumika kuwajengea uwezo watoto wa Mabaraza hayo.
Bi. Magwiza aliongeza kuwa Watoto hawa walikuwa wanafundishwa kulingana na utashi wa aidha mtalaam anayewaratibu au Shirika lilosimamia uanzishwaji wa Baraza na kuongeza kuwa jambo hili lileta utofauti wa uelewa na hata baadhi ya watoto kutofautiana kutoka mkoa mmoja hadi mwingine.
Aidha Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Save the Children Tanzania Bi. Neema Bwaira wakati akitoa hotuba yake kwa Mgeni rasmi ameiomba Serikali isaidie kuhamasisha Halmashauri na Taasisi za Serikali nchini kutenga Bajeti kwa ajili ya kushughulikia masuala ya watoto hapa nchini.
Wakati huo huo Katibu Tawala Mkoa wa Geita Bw. Denis Bandisa mara baada ya uzinduzi wa Kitini hicho ameziagiza Halmashauri zote Mkoani Geita kutenga Bajeti kwa ajili ya mabaraza ya watoto na kuhakikisha masuala ya watoto yanashamiri katika mipango yao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Bw. Joel Festo amesema uzinduzi wa Kitini hiki utawezesha Baraza lake na watoto nchini kuwafundisha kujua ni nini cha kufanya katika wajibu wao kama raia wa Tanzania lakini pia kuleta mabadiliko makubwa kwa watoto wa Tanzania.
Uzinduzi wa Kitini hiki sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo uadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 16, Juni na tayari Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Save the Children wametoa mafunzo ya kitini hiki kwa Baraza la Watoto la Taifa katika mfululizo wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Mkoa wa Geita kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto.