Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na Balozi wa India anayemaliza muda wa uwakilishi nchini, Mhe. Sandeep Arya (wa pili baada ya aliyevaa tai nyekundu) jijini Dar Es Salaam. Mhe. Waziri alimuandalia chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Mhe. Balozi. Katika chakula hicho, Prof. Kabudi alishukuru misaada ya maendeleo inayotolewa na Serikali ya India katika sekta mbalimbali zikiwemo za maji, elimu, nishati na afya. Mhe. Waziri pia alimuhakikishia Mhe. Balozi kuwa Serikali itatoa ushirikiano kwa Balozi mpya atakayekuja kuchukua nafasi yake nchini.
Prof. Kabudi akiwa na ujumbe wake wakati wa chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga Balozi wa India anayemaliza muda wa uwakilishi nchini. |