Home Mchanganyiko SULEIMAN MATOLA AIKIMBIA LIPULI FC NA KUJIUNGA NA TIMU YA POLISI TANZANIA

SULEIMAN MATOLA AIKIMBIA LIPULI FC NA KUJIUNGA NA TIMU YA POLISI TANZANIA

0

Na Asha Said, DAR ES SALAAM
TIMU ya Polisi Tanzania ya Kilimanjaro itakayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu ujao imemtambulisha rasmi Selemani Matola kuwa kocha wake msaidizi.
Matola ambaye ni kiungo wa zamani wa Simba, alikuwa kocha msaidizi wa Lipuli FC kwa misimu miwili iliyopita akiiwezesha kumaliza nafasi ya sita na kufika fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) msimu uliopita.
Polisi imepanda Ligi Kuu baada ya kuongoza Kundi B ikiungana na Namungo FC ya Lindi iliyoongoza Kundi A zikichukua nafasi za African Lyon na Stand United zilizoshuka moja kwa moja kutoka Ligi Kuu.

Polisi ilipanda Ligi Kuu ikiwa chini ya Kocha Mbwana Makatta ambaye baada ya hapo ameondolewa na sasa timu hiyo itaendelea kutafuta kocha Mkuu mwingine atakayefanya kazi na Matola.