Home Mchanganyiko MAMLAKA YA BANDARI YATEKELEZA KWA VITENDO KAULIMBIU YA “TANZANIA YA VIWANDA”, ...

MAMLAKA YA BANDARI YATEKELEZA KWA VITENDO KAULIMBIU YA “TANZANIA YA VIWANDA”, UJENZI WA BANDARI YA KABWE MKOANI RUKWA WASHIKA KASI

0

Meneja wa Bandari katika ziwa Tanganyika (TPA) Bw. Ajuaye Kheri Msese akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la mradi mjini Kabwe.

……………………………………………………

Kauli ya Serikali ya awamu ya tano ya inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli isemayo “Tanzania ya viwanda” imeendelea kuelekeza na kuamsha ari ya taifa kupiga hatua ya maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi huku miradi mikubwa na midogo ikitekelezwa kwa kasi nchini.

Kutokana na msisitizo wa kauli hiyo Mamlaka ya Bandari nchini (TPA),imeamua kujenga bandari ya kisasa wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa katika mji wa Kabwe uliopo kwenye mwambao wa ziwa Tangayika huku ikifanya hivyo pia katika maziwa makuu yake mengine ya Victoria na Nyasa

Meneja wa Bandari katika ziwa Tanganyika (TPA) Bw. Ajuaye Kheri Msese ,amesema  bandari hiyo licha ya kuwa kitega uchumi cha nchi vile vile wananchi watakuwa wanufaika wakubwa hususan wanaofanya shughuli zao kati ya Moba nchini DRC Congo na hapa Tanzania na maeneo mengine.

Bw. Msese anasema (TPA) imeamua kujenga bandari hiyo ya Kabwe ili kuwaondolea adha wananchi ambao wamekuwa wakitembea majini wakati wa kushuka au kupanda kwenye vyombo vyao vya usafiri kwa kukosa gati.

Mmoja wa wafanyabiashara katika mji wa Kabwe Bw.Ibrahim Mouti ambaye anatumia usafiri wa majini anasema kuwa, Kutokuwepo kwa gati kubwa kunaleta adha kubwa katika upakiaji wa mizigo.

“Unapakia mzigo kiasi kidogo kisha unalihamisha boti kwenda kwenye kina kirefu, alafu mnaanza kupakia tena kwa kusogeza na boti lingine jambo ambalo ni hatari sana”

Baadhi ya vijana waliobahatika kupata ajira katika ujenzi wa mradi wa bandari hiyo ,wamesema wanaishukuru serikali kwa utekelezaji wa mradi huo ambao umeongeza kipato chao cha kila siku kutokana na malipo yao ya mishahara katika kazi hiyo

Mradi wa Bandari ya Kabwe unajumuisha Usanifu, ujenzi wa Gati, Jengo la kupumsikia abiria, Jengo la Mgahawa, Ofisi, Ghala la kuhifadhia mizigo, Nyumba za wafanyakazi na uzio ukigharimu zaidi ya  shilingi Bilioni 7.4. Amesema Msese.

Mkandarasi wa mradi huo M/S Sumry’s Enterprises Ltd  anaendelea na ujenzi ambapo kazi ilianza Aprili 1, 2018 akiwa ametekelezwa kwa asilimia 40% na muda wa ujenzi ni miezi 24

Nkasi ni moja kati ya wilaya tatu zinazounda mkoa wa Rukwa ikiwemo,Sumbawanga na Kalambo.

Meneja wa Bandari katika ziwa Tanganyika (TPA) Bw. Ajuaye Kheri Msese akiwaonesha waandishi wa habari shughuli mbalimbali zinazofanyika katika mradi huo.

Mmoja wa wafanyakazi katika mradi huo akiwaelezea waandishi wa habari namna wanavyofanya kazi kwenye meadi huo ambao kwa kiasi fulani umeongeza kipato chao cha maisha.

Baadhi ya mafundi wakiendelea na kazi.

Baadhi ya majengo yakiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Mitambo mbalimbali imesimikwa katika mradi huo kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.

Baadhi ya majengo yakiwa katika hatua mbalimbali.

Mafundi mchundo wakiwa kazini katika mradi huo.

Baadhi ya nguzo zikiwa tayari kwa ajili ya kuzamishwa kwenye maji.

Moja ya mashine kubwa ikiendelea na kazi katika mradi huo.

Afisa Mwasiliano Mwandamizi Mamlaka ya Bandari TPA Bw. Leonard Magomba katikati akizungumza na baadhi ya wakandarasi na maofisa wa bandari Kabwe.