Home Biashara Mawakala wa Tigo Pesa wajishindia mamilioni

Mawakala wa Tigo Pesa wajishindia mamilioni

0

Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kukabidhi zawadi kwa mawakala wa Tigo Pesa waliofanya vizuri katika promosheni inayojulikana ‘Wakala Cash In Promotion’. Kushoto ni Suleiman Hussein na kulia ni Vicky Ibrahim wote wakiwa ni washindi wakubwa kutoka kanda ya Pwani.

Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 3.5 Suleiman Hussein ambaye ni mmoja kati ya washindi wakubwa wawili wa promosheni ya ‘Wakala Cash In Promotion’ kutoka kanda ya Pwani.

Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 2.5 Vicky Ibrahim ambaye ni mmoja kati ya washindi wakubwa wawili wa promosheni ya ‘Wakala Cash In Promotion’ kutoka kanda ya Pwani.

Kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha (Katikati) akiwa na washindi wa ‘Wakala Cash In Promotion’ kutoka kanda ya Pwani Vicky Ibrahim (kulia) na Suleiman Hussein (kushoto) muda mfupi baada ya kuwakabidhi zawadi zao za fedha baada ya kuibuka washindi.

…………………………………………………………..

Na Mwndishi Wetu
Zaidi ya mawakala 200 wa huduma ya Tigo Pesa, wamejishindia zawadi za fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 160 kwenye promosheni ya mwezi mmoja inayojulikana kama ‘Wakala Cash In Promotion’.
Promosheni hiyo ya nchi nzima iliyozinduliwa mwezi Mei mwaka huu, ililenga kuwahimiza Mawakala wa Tigo Pesa nchini kufanya miamala kwa wingi ili kuweza kujishindia zawadi za fedha taslimu.
Akiwakabidhi zawadi washindi wa promosheni hiyo, kaimu mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa Angelica Pesha alisema, kampuni ya Tigo inathamini juhudi kubwa zinazofanywa na mawakala na kuongeza kuwa promosheni hiyo ililenga kuwazadia mawakala kutokana na kazi nzuri wanayoifanya.
“Kampeni hii siyo tu inaonyesha dhamira yetu ya kuwekeza kwenye biashara lakini pia adhma yetu ya kugawana tunachokipata kutokana na biashara tunayofanya pamoja na wadau wetu. Promosheni hii ni fursa nyingine ya kuwazawadia mawakala wetu fedha taslimu na bonasi ambazo tunawaamini zitawapa moyo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kuendelea kufikisha huduma jumuifu za kifedha kwa wananchi wengi zaidi,” alisema
Kwa mujibu wa Pesha, pamoja na washindi wengine, washindi wawili wakubwa kutoka kila kanda walipatikana ambao ni Suleiman Hussein na Vicky Ibrahim kutoka Kanda ya Pwani, Peter Myovela na Stivin Katoto kutoka kanda ya Kusini, Anton Masawe na Athuman Mbwana kutoka kanda ya Kaskazini pamona na Harry Lwila na Joseph Kabeba kutoka Kanda ya Ziwa.
“Pamoja na washindi 2000 ambao wamejinyakulia zawadi mbali mbali za fedha taslimu kutokana na juhudi zao, tumepata washindi wengine wawili wakubwa kutoka katika kila kanda ambao kwa jumla wao ni 8 ambao wameweza kujishindia shilingi milioni 12 zaidi kutokana na jitihada zao. Tunawapongeza sana Mawakala wote ambao wamefanya vizuri na kujishindia zawadi na kwa wale ambao wahakuweza kushinda waongeze bidii ili waweze kuwa washindi katika promosheni zijazo,” alisema.
Akipokea zawadi ya shilingi milioni 3.5, Suleiman Hussein ambaye ni Wakala kutoka Kanda ya Pwani alisema “Napenda kuishukuru sana kampuni ya Tigo. Promosheni hii inaonyesha ni kwa kiasi gani sisi mawakala ni kiungo muhimu kwenye huduma nzima ya Tigo Pesa. Kuibuka mshindi kwenye promosheni hii ni rahisi sana kwa kuwa unahitajika kufanya kazi kwa bidii tu. Nawashauri Mawakala wenzangu wafanye kazi kwa bidi kwani Tigo Pesa inalipa,”
Vicky Ibrahim, Wakala aliyejishindia shilingi milioni 2.5 alisema amefurahi kuwa mshindi wa zawadi hiyo na kuwataka wanawake kuwa mawakala wa Tigo Pesa na wale ambao tayari ni mawakala kuwekeza zaidi na kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa Tigo Pesa.
“Tigo Pesa imetuwezesha sisi wanawake kujiajiri na kuboresha maisha yetu. Nawashauri wanawake wenzangu kujiajiri au kujiongezea vipato vyao kupitia Tigo Pesa. Kwa kuwa Mawakala pia wanaweza kujishindia zawadi kupitia promoshei hii kama ambavyo mimi nilivyojishi,” alisema