Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mh.Said Mtandaakizungumza na waandishi wa habari mjini Nkasi wakati waipotembelea ujenzi wa miundombinu ya afya wulayani humo.
………………………………………………..
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mh.Said Mtanda amesema tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo mwaka 1979 haikuwahi kuwa na chumba cha kuhifadhia maiti, lakini kutokana na jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk John Pombe Magufuli, Nkasi imekuwa kati ya wilaya zilizofanya vizuri katika maendeleo katika sekta ya afya.
Akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kuripoti kuhusu miradi ya maendeleo wilayani humo amesema Kituo cha afya cha Nkomolo kimepata chumba cha kuhifadhia maiti na majokofu sita ambayo awali hayakuwepo na wakazi wa wilaya ya hiyo walikuwa wanalazimika kwenda mpaka Sumbawanga kwa ajili ya kuhifadhi maiti” amsema Mtanda.
Ameongeza kuwa wilaya ya Nkasi imekamilisha ukarabati wa kituo cha Afya cha Nkomolo na ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo unaendelea kwa kasi.
Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli imewafanyia mambo makubwa wananchi wa wilaya ya Nkasi kutokana na utekelezaji wa miradi hii ambayo ujenzi wake utagharimu sh.Bilioni Mbili.
” Hospitali ya Wilaya inajengwa kwa gharama sh. Bilioni 1.5 na majengo ya kituo cha Afya Nkomolo yamejengwa na kukarabatiwa kwa gharama ya sh. Milioni 500 ambayo yamekamilika na kituo cha afya tayari kinatoa huduma. “Amesema Mtanda
Amesema kuwa mara baada ya kukarabati kituo hicho cha Afya wameweza kutoa huduma ya Upasuaji kwa watu sita kwa wakati mmoja jambo ambalo halikuwepo hapo awali.
Amesema kuwa kuwa kwa kipindi chote hicho Wilaya hiyo ilikuwa haina Hospitali ya Wilaya lakini katika awamu hii ya tano chini ya Rais Magufuli, Nkasi inakwenda kwa kasi na imepata Hospitali mpya.
Naye Mganga Mkuu wa kituo cha afya Nkomolo Everada Sanane amesema bado kuna uhitaji wa watumishi kutokana na idadi ya wagonjwa inavyoongezeka na ameishukuru serikali kwa hatua ilizopiga katika kuboresha sekta ya afya Wilayani humo.
MKUU wa Wilaya ya Nkasi, Mh.Said Mtandaakifafanua mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari wakati akitoa mwelekeo wa wilaya hiyo katika sekta ya afya.
Jengo la wazazi kituo cha afya cha Nkomolo mjini Nkasi.
Jengo la Ipasuaji linavyoonekana
MKUU wa Wilaya ya Nkasi, Mh.Said Mtandaakizungumza na baadhi ya wazazi waliojifungua katika kituo hicho cha afya mjini Nkasi.
MKUU wa Wilaya ya Nkasi, Mh.Said Mtandaakionesha baadhi ya mitambi iliyopo katika jengo la akina mama ambamo watoto huwa wanawekwa baada ya kuzaliwa.
Baadhi ya vitada katika wodi ya wazazi.
MKUU wa Wilaya ya Nkasi, Mh.Said Mtanda akionesha Mochwari kwa ajili ya kuhifadhia maiti katika kituo cha afya cha Nkomolo mjini Nkasi.
Picha mbalimbali zikionesha ujenzi wa majengo ya hospitali ya wilaya ya Nkasi unavyoendelea.
MKUU wa Wilaya ya Nkasi, Mh.Said Mtand akionesha majengo mbalimbali yanayojengwa katika eneo la hospitali ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.
MKUU wa Wilaya ya Nkasi, Mh.Said Mtanda akionesha jengo litakalohusika na mionzi katika hospitali hiyo ya wilaya.
MKUU wa Wilaya ya Nkasi, Mh.Said Mtanda akiongozana na waandishi mbalimbali wakati wakitembelea ujenzi wa majengo ya hospitali ya wilaya ya Nkasi.