Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma , Bw. Ajuaye Kheri Msese amesema Bandari ya Kigoma inayo miundombinu mingi kwa ajili ya kukarabati na kufanyia ukaguzi wa meli pale huduma hiyo inapohitajika kwa wamiliki wa meli kutoka ndani ya nchi na nchi jirani.
Bw. Msese amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika bandari ya Kigoma ili kujionea shughuli mbalimbali za bandari hiyo iliyopo katika ziwa Tanganyika mkoni Kigoma.
Meneja Msese amesema wanayo (Slipway) Chelezo iliyoujengwa na wajerumani yapata miaka 90 iliyopita, ni (Slipway) ndefu kuliko zote katika ziwa Tanganyika hivyo inao uwezo wa kupandisha meli kubwa, ndefu na ndogo ili kufanyiwa marekebisho na ukaguzi.
“Kwa mwaka tunao uwezo wa kuhudumia meli zipatazo kumi na kuendelea kulingana na mahitaji ya wateja wetu, na hivi karibuni kuna meli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itapandishwa kwenye (Slipway) Chelezo ili kufanyiwa matengenezo” Amesema Msese.
Meli moja hupandishwa kwenye (Slipway) kwa gharama ya dola 200 ili kuanza matengenezo na huchajiwa kiasi cha dola 400 kwa siku na gharama halisi inategemea meli itakaa kwa muda gani wakati iko kwenye marekebisho.
Amewaasa wamiliki mbalimbali wa meli katika ziwa Tanganyika kutoka nchini Tanzania na nchi jirani kama vile DRC Congo, Burundi za Zambia kutumia (Slipway) ya Bandari ya Kigoma kwa sababu gharama zake ni nafuu na uwezo wa kubeba meli ndefu, kubwa na ndogo pia.
Chelezo (Slipway) Bandari ya Kigoma inavyoonekana kwa juu katika bandari hiyo.
MV Mwongozo ambayo inatarajiwa kufanyiwa ukarabati itapandishwa kwenye (Slipway) hiyo kama inavyoonekana.
Moja ya Mashine inayoondoa mchanga kuongeza kina bandarini inayoitwa Water Masrter ikiwa bandarini hapo kwa ajili ya kazi hiyo.
Hii ni miundombinu ya kupokelea mafuta kutoka kwenye meli na matanki ya kuhifadhia mafuta iliyopo katika bandari ya Kigoma.
Bandari ya Kigoma inavyoonekana kwa juu.
Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma , Bw. Ajuaye Kheri Mseseakiwaelezea waandishi wa habari kuhusu meli mbalimbali za mizigo zinazoleta na kuchukua mizigo kutoka nchi jirani za Burundi, DRC Congo na Zambia.
Moja ya mashine ya kupakia na kushusha mizigo ikiendelea na kazi ya kushusha mizigo kutoka kwenye meli ya MV Kiriri kutoka nchini Burundi.
Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma , Bw. Ajuaye Kheri Msese akionyesha shehena ya Makasha (Container) ya kubebea mizigo yanayoshushwa na kupakiwa kwenye meli bandarini hapo.
Baadhi ya mizigo ikiwemo Saruji ikiwa tayari kusafirishwa kwenye Burundi.
Shehena ya saruji ikiwa tayari kwa kupakiwa kwenye meli.
Moja ya mizani za kupimia mizigo zilizopo bandarini hapo.