Ikiwa Tanzania inaungana na mataifa mengine Ulimwenguni kuadhimisha siku ya kupinga ajira za utotoni, Huko mkoani Njombe serikali imesema zaidi ya matukio ya 180 ya ukatili yamefanywa dhidi ya watoto huku takwimu za mwaka jana zikionesha watoto takribani 302 walifanyiwa ukatili.
Kufuatia matukio hayo takribani kesi 31 zimefunguliwa na watuhumiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili kuhusiana na kufanya vitendo vya kikatili kwa watoto ikiwa ni pamoja na Ajira za utotoni,ubakaji, ulawiti, kukatishwa masomo na mengine mengi ambayo yanamnyima haki mtoto.
Akizungumzia matukio hayo na hatua zinazochukuliwa na serikali kudhibiti vitendo hivyo afusa ustawi mkoa wa Njombe Teresia Yomo amesema serikali imejitahidi kwa kiasi kikubwa kudhibiti vitendo vinavyo kiuka haki za mtoto ikiwa ni pamoja na kutoa elimu jambo ambalo limekuwa na matokeo chanya kwa jamii za watu wa Njombe .
Ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mkoani Njombe limetajwa kusababishwa na mambo mengi huku imani potofu,mila mbaya na uelewa mdogo zikitajwa kushika kasi zaidi hali ambayo inamsukuma Wema Mbanga na Perto Mkongwa kuiomba serikali kutumia vituo vya yatima kuwasaidia watoto waliotelekezwa na wazazi wao.
Mtanado huu umezungumza na mtoto Aleni jonas mwenye umri wa miaka 14 ambaye ametoroka nyumbani kwao mwaka jana na kuja mjini kutafuta kazi ambapo amefanikiwa kupata kazi ya kuuza duka .