Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera akizungumza na wandishi wa habari walipomtembelea ofisini kwake leo kujua mipango mbalimbali ya maendeleo kwa mkoa huo.
……………………………………………………………………………
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera amesema licha ya kutafsiriwa vibaya kwenye baadhi ya vyombo vya habari,hatasita kuchukua hatua kwa watu wote wanaofanya kampeni za kupita nyumba kwa nyumba kuwashawishi wananchi kwa lengo la kufanikisha mambo yao ya siasa.
Mh. Juma Homera ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujua mikakati na mipango ya maendeleo ya mkoa huo katika kuwaletea maendeleo wananchi.
“Nawaonya wananchi hususan wanasiasa kuacha kufanya siasa za nyumba kwa Nyumba kwa sababu muda wa siasa hizo bado na msajiri wa vyama vya saiasa alishapiga marufuku mikutano hiyo kasoro ile ya ndani tu ,vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.
Homera amesema marufuku hiyo ni kwa vyama vyote vya kisiasa nchini ikiwemo CCM na vyama vingine vyote vya siasa.
“Hii ni Juni,wanasiasa wakae wasubiri muda mwafaka ufike wafanye wanachokifanya na tena ni kwa mujibu wa sheria,si kiholelaholela,” amesema.
Wakati Huo huo Homera amewataka watanzania kutenga bajeti na muda wa kufanya utalii katika Hifadhi ya wanyamapori ya Katavi ambayo ni ya tatu kwa ukubwa baada ya Serengeti na Selous.
Mkuu huyo wa mkoa wa Katavi amesema Hifadhi ya Serengeti ina wanyama wengi na vivutio mbalimbali kwa watalii zikiwemo hoteli na Camp za viwango vya kimataifa.
Amepongeza Camp ya Katuma Bush Lodge iliyopo ndani ya hifadhi ya Katavi kwakuwa Camp yenye ubora na viwango vya kimataifa kwa mgeni yeyote anayeweza kufikia katika Camp hiyo.
Amewakaribishwa wageni kutoka mataifa mbalimbali na watanania kutalii katika hifadhi ya Katavi ikiwa ni pamoja na kuitembelea hifadhi hiyo bila kukosa kwakuwa ina wanyama wa kila aina wakiwemo Tembo, Twiga, Pundamilia, Nyati, Viboko, Mamba, Swala Simba na wanyama wengine wengi.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera akipokelewa na wahifadhi mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori ya Katavi wakati alipowaongoza waandishi wa habari kutembelea vivutio vya hifadhi hiyo leo.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera akisaini kitabu cha wageni.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera akisaini kitabu cha wageni kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma , Bw. Ajuaye Kheri Msese
Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma , Bw. Ajuaye Kheri Msese akisaini kitabu cha wageni.
Msimamizi wa Shughuli za Utalii katika Hifadhi ya Wanyamapori ya Katavi Bw. Anthony Shirima akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliotembelea katika hifadhi hiyo leo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika ofisi za hifadhi hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera akiongoza waandishi wa habari kutembelea hifadhi ya wanyamapori ya Katavi na kujionea vivutio mbalimbali katika hifadhi hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliotembelea Camp ya Katuma Bush Lodge iliyopo ndani ya hifadhi ya Katavi
Picha zikionyesha Samani mbalimbali zilizopo katika moja ya nyumba zilizopo katika Camp ya Katuma Bush Lodge iliyopo ndani ya hifadhi ya Katavi
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliotembelea Camp ya Katuma Bush Lodge iliyopo ndani ya hifadhi ya Katavi
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh. Juma Homera akitoa maelezo kwa waandishi wa habari waliotembelea mto wenye viboko uliopo katika hifadhi hiyo kwa mbali kinachoonekana nyuma ya Mkuu wa mkoa siyo tope ni viboko wakiwa walelala katika tope hilo.
Mmoja wa viboko akiwa amejituliza katika dimbwi la maji kwenye mto huo.
Moja ya nyumba katika Camp ya Katuma Bush Lodge iliyopo ndani ya hifadhi ya Katavi mkoani Katavi.
Picha ikionyesha baadhi ya tembo wakijipatia chakula katika hifadhi hiyo.