Home Michezo Shule ya Southern Highlands Mafinga kukabidhi Azimio la Dunia kwa Mawaziri wa...

Shule ya Southern Highlands Mafinga kukabidhi Azimio la Dunia kwa Mawaziri wa JPM

0

Mkurugenzi wa shule ya Southern Highlands Mafinga Mary Mungai (wa tano kulia) akiwa na wazazi wa na marafiki wa wanafunzi Mariam Wambura na Stephen Sanga ambao waliwakilisha shule za Tanzania katika kongamano la dunia la mazingira nchini Finland wa kwanza kulia ni mkuu wa msafara wa wanafunzi hao Kitova Mungai .

Wanafunzi wa  shule ya  Southern Highlands Mafinga  na viongozi  wao  wakiwa  katika eneo  lilolohifadhiwa katika  misitu ya  sao Hill Mufindi  wakijifunza jinsi ya  utunzaji wa mazingira

………………….

NA Francis Godwin,Iringa

Uongozi wa shule ya Southern Highlands Mafinga mkoani Iringa umesema unakamilisha utaratibu wa kukabidhi azimio la dunia lililokabidhiwa kwa wanafunzi wawili wa darasa la saba katika shule hiyo Mariam Wambura na Stephen Sanga ambao waliliwakilisha shule za Tanzania nchini Finland katika Tanzania kongamano mazingira kwa la shule za msingi duniani .

Mkuu wa msafara wa wanafunzi hao nchini Finland ,Kitova Mungai ambae ni mmoja wa mkurugenzi wa shule hiyo alisema kuwa wanafunzi hao Mariam Wambura na Stephen Sanga wamerejea nchini baada ya kushiliki katika kongamano hilo la siku 10 nchini Finland .

Kuwa kongamano hilo la siku kumi la wanafunzi kuhusu utunzaji mazingira limehitimishwa kwa kutoa azimio kwa wanafunzi kuhusu utunzaji wa mazingira azimio hilo ambalo litawezesha dunia kuwa katika hali nzuri ya ustawi wa mazingira duniani.

Kuwa azimio hilo limelenga kuhamasisha shule na jamii kuendelea kutunza mazingira ili kuwezesha kizazi cha baadae kuishi katika mazingira salama yasiyo na uharibifu wa mazingira.

“Tumekuwa tukiwafundisha masomo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira na wamekuwa wakiotesha miche ya miti na kuisambaza maeneo mbali mbali ya shule ” alisema Mungai

Kuwa Katokana na kazi hiyo ya utunzaji mazingira ndio iliyowezesha shule hiyo wanafunzi wake kuteuliwa na waandaaji wa kongamano hilo kwenda nchini Finland kushiriki kongamano hilo la dunia kwa niaba ya shule zote Tanzania.

Hata hivyo alisema wanakusudia azimio hilo ambalo walipewa na waandaaji wa kongamano hilo kuliwasilisha serikalini ili kulisambaza kwenye shule zote nchini kwa kupitia viongozi wa serikali ya Tanzania ili shule zote kuweza kutekeleza maagizo yaliyitolewa kwenye kongamano hilo la dunia.

Mungai alisema kuwa azimio hilo limegawanyika katika sehe kuu tatu ikiwemo ya kuangalia uwezekano wa kuondoa kaboni katika hewa ili kuona jinsi ya kuidaka hewani na kuihifadhi sehemu ili isilete madhara mbeleni , sehemu ya pili ya azimio ni kupunguza kaboni hiyo katika mazingira yetu na sehemu ya tatu ni kuweka utaratibu mzuri wa kuwasiliana kati ya wanafunzi wa Tanzania na wale wa nchi nyingine .

” Azimio   hili  tunategemea kulikabidhi kwa mawaziri wa  serikali ya Rais Dkt John Magufuli   akiwemo  waziri wa  elimu ,waziri wa TAMISEMI na  waziri  wa mazingira   ili  kuweza   kulisambaza azimio   hili kwa shule  zote za  msingi nchini na  kwenye Halmashauri na mikoa ili  kuanza  utekelezaji wa  uhifadhi wa mazingira ”  alisema

Kuwa  wakiwa katika  kongamano hilo la  wanafunzi  duniani  walipata nafasi ya kushiriki  kongamano jingine la  kuangalia  viwanda   duniani vinafanyaje katika maeneo yao  kuhakikisha  wanazalisha  bila  kuharibu mazingira  kongamano ambalo baloz wa Tanzania anayewakilisha  nchi kama  tano  ikiwemo ya Sweden  nchini Dr. Wilbrod Peter Slaa  alikuwa ni  miongoni mwa  washiriki wa  kongamano hilo kubwa .

Kwa  upande wake  mkurugenzi mtendaji wa shule  hiyo Mary Mungai alisema  kuwa  kutokana na heshima kubwa  ambayo shule  yake  imeipata ya  kuwakilisha Taifa  katika kongamano hilo la  dunia  watahakikisha  wanakuwa  mabalozi  wazuri  wa  kuelimisha jamii  juu ya  utunzaji wa mazingira  na  kuwa  azimio  hilo wataanza  kulifanyia kazi wao  ili  wengine wafike   kujifunza .

Wanafunzi walioshiliki katika  kongamano hilo Mariam na Stephen  walisema kuwa   tofauti ya nchini ya Finland na  Tanzania  katika  uhifadhi wa mazingira ni  kubwa kwani  wakiwa katika kongamano hilo   waliweza  kujifunza na  kuzunguka  mitaa mbali mbali  kuona jinsi  wananchi wa Finland  wanavyozingatia  uhifadhi wa mazingira kwa  kutenga vyombo vya  kuhifadhi taka  ngumu ,taka laini na taka nyingine  na sio kama  ilivyo Tanzania kwa maeneo mengi kuwa na chombo kimoja cha taka kinachotupwa  taka  zote .

Pia  walisema   kwa  upande wa vyombo  vya  moto  mfano magari  kuwa  nchini Finland magari yao yanatumia umeme na sio mafuta  kama  ilivyo Tanzania  na  kuwa wanatumia magari hayo yanayotumia umeme   kama njia ya  kulinda   usafi  wa mazingira yao.