Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma , Bw. Ajuaye Kheri Msese akiwaelezea waandishi wa habari utekelezaji wa mradi wa Bandari ya Kagunga iliyopo Kigoma Vijijini ambayo kwa kiwango kikubwa imekamilika majengo ya abiria na kuhifadhia mizigo, Nyumba za wafanyakazi na Gati la Kisasa ambalo linaweza kupokea meli tatu kwa wakati moja.
Bandari hiyo ni ya kimkakati kwa sababu itahudumia mizigo yote inayokwenda nchi ya Burundi na itawapunguzia gharama za usafirishaji kutoka Dar es salaam au Kigoma sasa watapokelea mizigo yao yote katika bandari hiyo mara itakapoanza kufanya kazi.
Bandari ya Kagunga ilianza kujengwa mwezi Agosti mwaka 2015 na kwa sasa imekamilika kinachoendelea ni ujenzi wa barabara kutoka katika mpaka wa Burundi kwenda bandarini hapo yenye urefu wa zaidi ya kilomita moja, Pamoja na ujenzi wa soko.
Injinia wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma Nyakato Mwamnana akifafanua baadhi ya mambo kuhusu mradi wa ujenzi wa bandari ya Kagunga katika ziwa Tanganyika ambayo itasaidia sana nchi ya Burundi na maeneo mengine kupata huduma ya usafirishaji wa mizigo yao kutoka bandari ya Dar es salaam, Kigoma na maeneo mengine ya ziwa Tanganyika.
Bw. Yudas Sukanyi Mkuu wa Usalama Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma akielezea namna Mamlaka ya bandari Kigoma inavyoshirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika kuimarisha usalama kwenye badari zake zote kwenye ziwa Tanganyika .
Baadhi ya majengo yanavyoonekana bandarini hapo.
Hili ni eneo la kupumzikia abiria na kusubiri taratibu mbalimbali za usafiri.
Picha mbalimbali zikiionyesha Bandari ya Kagunga kwa juu ni bandari iliyojengwa kwa viwango vya kisasa kabisa.
Baadhi ya waandishi wakimsikiliza Injinia wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma Nyakato Mwamnana wakati akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa bandari hiyo.
Ujenzi wa Soko ukiendelea
Baadhi ya mafundi kutoka kampuni ya Essau Construction wakiendelea na ujenzi wa soko la Kagunga.
Injinia wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma Nyakato Mwamnana akitoa maelekeza kwa mafundi wa kampuni ya ujenzi ya Essau Construction wanaojenga soko la Kagunga.
Injinia wa Kampuni ya ujenzi wa Essau Construction injinia Adrian Clement akitoa maelezo kwa Injinia wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma Nyakato Mwamnana kuhusu maendeleo ya ujenzi huo.
Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Tanganyika(TPA) Kigoma , Bw. Ajuaye Kheri Msese akitoa maelezo kwa Injinia Adrian Clement kutoka kampuni ya Essau Construction inayojenga soko la Kagunga.