Home Mchanganyiko HAFLA YA CHAKULA CHA YATIMA

HAFLA YA CHAKULA CHA YATIMA

0

Mjumbe wa Baraza la Masheikhe Mohamed Ruiyal (kushoto) na Mjumbe wa Halmashauri ya BAKWATA Mkoa wa Mwanza, Sheikh Rajabu Rajabu (kulia) wakishiriki kula chakula na watoto yatima kwenye sikukuu ya Idd el Fitri jana.

Kaimu Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza Sheikhe Hassan Kabeke (kulia) akiwanawisha watoto yatima tayari kwa ajili ya kula chakula kilichoandaliwa kwa ajili yao wakati wa sikukuu ya idd jana.

Mfanyabishara Zakaria Nzuki akizungumza kabla ya hafla ya chakula alichokiandaa kwa kushirikiana na BAKWATA Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya watoto yatima wakati wa sikukuu ya Idd El FitriĀ 
Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula naye akishiriki kunawisha watoto yatima kwa ajili ya kula chakula cha pamoja kilichoandaliwa na mfanyabishara Zakaria Nzuki kwa kushirikiana na BAKWATA kwa ajili ya yatima hao jana.