Home Michezo NEYMAR MAJANGA JUU YA MAJANGA

NEYMAR MAJANGA JUU YA MAJANGA

0

**********************************************

Imethibitishwa kuwa Neymar ataikosa michuano ya Copa America baada ya kupata majeraha kwenye Mchezo wa kirafiki dhidi ya Qatar, ambapo Brazil waliibuka na ushindi wa 2-0.

Neymar amekuwa ni mchezaji ambaye anaumia kila kukicha na wachambuzi wengi wa soko barani ulaya wanadai ni kutokana na uchezaji wake.

Hivi karibuni pia Neymar alikumbwa na kashfa ya ubakaji nchini Ufaransa.

Ikumbukwe mwaka juzi Neymar alipatwa na majeraha ambayo yalimkalisha nje kwa muda mrefu na pakawa na hatihati ya kutoshiriki michuano ya kombe la Dunia huko Russia vilevile msimu ulioisha hivi karibu mchezaji huyo alikosa mechi kadhaa kutokana na majeruhi.