Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya True Vision Production wakiwasaidi watoto wenye ulemavu wakati wa ziara yao
David sevuri akiwakabidhi wanafunzi wa shule ya msingi Jeshi la Uwokovu sehemu ya vyakula wakati wa ziara yao ya Kaole
Mbali na kuona sehemu za kale, vyakula pia vilikuwa sehemu ya ziara hiyo
Mmoja wa wanafunzi akichukua kumbukumbuku muhimu kama anavyoonekana
Ulikuwa ni wajibu wa TVP crew kuwahudumia kama Isaac Lukando anavyoonekana pichani
***********************************
Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya
Jeshi la Uwokovu wamefurahia safari yao ya
kwenda kutembelea sehemu za mji wa kihistoria wa
Kaole uliopo mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani, ikiwa
sehemu yao ya kujifunza kwa vitendo
walichokisoma darasani kwa kipindi cha miaka 7
kabla ya kumaliza elimu yao ya shule ya msingi
miezi michache ijayo.
Wakiambatana na wafanyakazi wa True Vision
Production (TVP) waliofadhili safari hiyo ya sehemu
ya kujifunza kwa vitendo (study tour), wanafunzi
hao wamesema wamepata faraja sana kupata
ufadhili wa safari hiyo.
Kilichowafurahisha zaidi ni wafanyakazi wa TVP
kujumuika nao, kuwahudumia wale wenye ulemavu
wa viungo na kula nao pamoja chakula cha mchana.
Wakiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzao, Noah
Michael (15) amesema wamejifunza biashara ya
utumwa ilivyoanza Pwani ya Afrika ya Mashariki,
kikubwa zaidi akiwaomba TVP kuendelea kujitolea
kwa wanafunzi wenye uhitaji.
“Tumejifunza mambo mengi, tumefurahia pia
chakula kitamu, kikubwa zaidi TVP tumekuwa nao
katika matembezi yetu, wametuletea chakula
mezani na kuwa sehemu ya walezi wetu,” amesema
Michael.
Naye Joyce Mahona (14) , mwenye ndoto ya kuwa
daktari, amesema amejifunza jinsi watumwa
walivyokuwa wanauzwa, ameona msikiti wa kwanza
kabisa kujengwa katika karne ya 13, kisima cha kale
na kuona makaburi wa watu wa kale.
Alanus Lugome amesema mbali ya kuona vitu vingi
vya kale, kikubwa zaidi kilichomshangaza ni kuuona
mti wa ubuyu wenye miaka zaidi ya 500.
Katika kudhihirisha ule usemi usemao ‘Disability is
not Inability (ulemavu sio sababu ya kushindwa au
kutojua kitu), wanafunzi hao walimshangaza
mtembeza watu maeneo ya kale (Tour Guider), Leo Tagalile kwa maswali mazuri waliyouliza wanafunzi juu ya mji huo wa kihistoria.
Miongoni mwa maswali waliyoyauliza ni pamoja na
kutaka kujua akina nani waliokuwa wenyeji wa eneo
hilo kabla ya ujio wa wakoloni, kwa nini paliitwa
Kaole na je mbuyu huo bado unatoa matunda licha
ya kuwa na umri wa miaka 500?.
Pia wanafunzi hao, mbali na kuiona bandari ya
kwanza katika Pwani ya Afrika ya Mashariki, pia
walitembelea jengo la The Caravan Serai,
lililojengwa mwaka 1870 kwa ajili ya kupokea
watumwa waliotoka sehemu mbalimbali kama vile
Kilwa Masoko kabla ya kuuzwa.
“Mmefanya kitengo kikubwa sana kwa sababu
wanafunzi wenye ulemavu wa viungo, huwa
hawaamini kama jamii nyingine inawakubali na
kuwathamini,”
“Siku zote wanajisikia faraja sana watu wengine
wanapojumuika nao sababu wengine hata jamii zao
zinawatenga,”
“Wao wamezoea kuwa karibu na jamaa zao na
walimu wao tu, wakitokea watu wengine tofauti
kama TVP na kuwa nao siku nzima, wao wanafarijika
sana,” amesema Anne Kibanga Mwamgunda,
mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, inayojumuisha
“TT
“Mbali ya kuwasaidia katika mitihani, pia itawapa
kumbukumbu muhimu katika maisha yao,”
amesema mwalimu Emmanuel Ibrahim.
Amesema mara ya mwisho wanafunzi wake
kutembelea Kaole ni miaka miwili iliyopita kwa
ufadhili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa
kampuni za IPP, marehemu Reginald Mengi.
Mmoja wa wafanyakazi wa TVP, David Sevuri
amesema wamejisikia faraja kuwasaidia wanafunzi
hao kwenda katika mji huo wa Pwani ya Bagamoyo
kama sehemu ya kujifunza kwa macho, baada ya
nadharia ya darasani.
“Tuliwahi kuwatumia wanafunzi watatu kutoka
shuleni kwenu kutengeneza tangazo la televisheni la
Haki Elimu, hivyo tukaona sababu nyingine ya kuwa
karibu na nyinyi,”amesema Sevuri.
TVP, inayojihusisha na utengenezaji wa Makala
maalumu za video (documentary) na matangazo ya
radio, ilitoa pia magunia ya unga, mchele na mafuta
kama sehemu ya msaada wa chakula kwa watoto
hao.