Home Biashara WAMILIKI WA MELI ZIWA VICTORIA WAASWA KUTUMIA CHELEZO (FLOATING DOCK) YA BANDARI...

WAMILIKI WA MELI ZIWA VICTORIA WAASWA KUTUMIA CHELEZO (FLOATING DOCK) YA BANDARI MWANZA KUFANYIA MATENGENEZO MELI ZAO

0

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Mwanza Bw. Geoffrey Lwesya  amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri katika ziwa Victoria kutumia Chelezo Karakana ya kutengenezea meli kwa lugha ya kitaalam (Floating Dock) iliyoko Bandari ya Mwanza Kusini mara wanapohitaji kufanya matengenezo au ukaguzi kwenye meli zao.

Akizungumza na Fullshangweblog katika mahojiano jana  Bw. Godfrey Lwesya, Amesema Huduma hiyo inapatikana katika bandari ya Mwanza Kusini na wanaweza kuitumia kwa kufanyia matengenezo ya meli na ukaguzi kwa gharama nafuu kabisa.

Lwesya ameongeza kwamba Mamlaka ya Bandari Mwanza imejitahidi kuwa na miundombinu muhimu ya kufanyia marekebisho ya meli ili kurahisisha uendeshaji wa shughuli mbalimbali za usafiri katika ziwa Victoria.

“(Floating Dock) hii inaweza kutumiwa na mtu yeyote au shirika lolote linalomiliki meli katika ziwa Victoria ili kufanya ukaguzi na matengenezo ya meli zao kwa gharama nafuu kabisa , hivyo tunawakaribisha sana kutumia huduma hii muhimu katika masuala ya marekebisho ya meli” Ameongeza.

Mamlaka ya Bandari nchini Tanzania inafanya juhudi mahsusi za kuweka sawa miundo mbinu yake katika bandari zote nchini ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali ya ujenzi wa Meli mpya, Kukarabati zilizopo, Kujenga Gati kubwa na za kisasa pamoja na kuboresha huduma za uendeshaji  ili kuboresha huduma za usafiri majini.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Mwanza Bw. Geoffrey Lwesya akifafanua mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari kuhusu Chelezo hiyo.

Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Mwanza Bw. Geoffrey Lwesya akiwaonyesha waandishi wa habari Chelezo hiyo (Floating Dock)haipo pichani.

Chelezo ya kufanyia marekebisho na matengenezo ya meli (Floating Dock) inavyoonekana kwa ndani.

Chelezo ya kufanyia marekebisho ya meli Floating Dock inavyoonekana kwa ndani.