Diwani wa Kata ya Buza James Mkude n Mwenye sharti jeusi na Mwenyekiti wa Jogging wilaya ya Temeke Mussa Mtulia wakiwa katika picha zenye matukio tofauti baada ya kushiriki katika chakula cha pamoja na kutoa zawadi mbalimbali kwenye kituo cha UMRA cha kulea watoto yatima kilichopo Yombo Buza Mtaa wa mashine ya maji Kata ya Buza leo.picha na Mpiga picha wetu.
**************************************
Mwandishi Wetu
WATANZANIA wameshauriwa wakati wote kutenda mema na zaidi kusaidia makundi Maalum pamoja na watoto yatima kwani kufanya hivyo Ndio sehemu ambayo inaweza kusaidia kukutanishwa na Mungu.
Ushauri huo umetolewa Dar Es Salaam leo na Diwani wa Kata ya Buza Manispaa ya Temeke James Mkude Baada ya kushiriki katika kula chakula cha pamoja kwenye kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika Mazingira magumu cha UMRA kilichopo Mtaa wa Yombo mashine ya maji ikiwa sehemu ya kusherekea sikuku ya Idd.
Diwani wa (CCM)ambaye alikua na Mwenyekiti wa Chama cha Jogging Wilaya ya Temeke ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasimi Mussa Mtulia ,James Mkude alisema katika wakati kama huu ndio muda muafaka wa kufanya jambo kwa ajili ya makundi Maalum ikiwa pamoja na yatima na alichokifanya kiongozi huyo wa Jogging ni cha kupongezwa.
“Haya yaliyoliyofanywa na Mwenyekiti Mtulia kwa ajili ya watoto wetu hawa ni mfano wa kuigwa kwani ameacha kukaa na familia Siku kama hii ya sikuku lakini ameamua kuja Kula chakula pamoja na yatima pamoja na kutoa sadaka yake hapa ” amesema Diwani mkude
Pia aliwataka viongozi wa Kata hiyo Chama na Serikali .kujenga tabia ya kutembelea kwenye Vituo vya watoto yatima ili kujua Mazingira na namna wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali.
Katika kuhakikisha watoto hao wanapata huduma bora alifanya harambee ya kuchangisha Fedha ambapo zilipatikana jumla ya shilingi laki 110,000 ambazo zitumika kununua gas pamoja na mahitaji mengine.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Jogging wilaya ya Temeke Mussa Mtulia,alisema kuwa pamoja na kushiriki katika vikundi vya kimichezo lakini pia wanashiriki katika kusaidia yatima na hata watoto wanaoishi kwenye Mazingira Magumu.
Amesema awali wazazi na Jamii walichukulia kama Jogging ni sehemu ya mambo yasiyofaa katika Jamii lakini ukweli michezo ni ajira,Afya,na tangu wameazisha mifumo hiyo matunda yanaonekana.
“Katika haya ambayo tunayafanya hata Serikali imekuwa ikiunga mkono haya tunayoyafanya na wanametambua rasim na ndio maana hata wanapomaliza kufanya matembezi mwisho wasiku wanashiriki katika shughuli za kijamii..” Amesema Mtulia
Pia alisema Mbali na.michezo lakini wamekuwa wakishiriki upandaji miti ,kufanya shughuli za usafi hivyo vijana na wazazi wasifikiri kwamba yanafanyika mambo ya hovyo nakwamba wanashiriki katika Jamii kama walivyofanya jana katika kituo hicho cha watoto yatima cha UMRA .
Naye Mlezi wa watoto hao na mmliki wa kituo hicho Rahma Juma alishukuru viongozi hao huku akibainisha baadhi ya changamoto ambazo anakabiliana nazo ikiwa pamoja na ukosefu wa sare za shule kwa watoto,pamoja na mambo mengine,nakutumia fursa hiyo kuomba misaada zaidi.