Waziri wa Madini Doto Biteko wa Kulia katikati akisisitiza jambo
wakati wa kikao chake na ujumbe wa Kampuni ya Ngwena Tanzania
Ltd “Ngwena” waliomtembelea waziri kupata ufafanuzi kuhusu
marekebisho ya sheria ya madini. Kulia kwake ni Katibu Mkuu wizara
ya Madini Prof. Simon Msanjila.
Waziri wa Madini Doto Biteko hayupo pichani akimsikiliza kwa makini
mmoja wa wajumbe wa Kampuni ya Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena”
waliomtembelea ofisini kwake kuja kupata ufafanuzi kuhusu
marekebisho ya sheria ya madini.
******************************************
Na Issa Mtuwa – Dodoma
Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Mwekezaji wa Kampuni ya
Ngwena Tanzania Ltd “Ngwena” na kufanya nao mazungumzo kuhusu
masuala mbalimbali, kubwa likiwa ni kutoa Ufafanuzi kuhusu Marekebisho
ya Sheria ya Madini inavyotoa fursa na mazingira mazuri ya uwekezaji
katika sekta ya madini hapa nchini.
Hatua hiyo inafuatia ombi la kampuni hiyo kuomba kukutana na waziri
Biteko ili kupata ufafanuzi wa moja kwa moja kutoka kwake kuhusu
mabadiliko hayo ya sheria.
Ombi la kutaka kuonana na waziri ni kutokana na kampuni ya Ngwena
kupata taarifa za upotoshaji na zisizo sahihi kuhusu mabadiliko ya sheria
ya madini yaliyofanywa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
kuhusu taratibu mbalimbali za uwekezaji na shuguli nyingine zinazo husu
sekta ya madini.
Upotoshaji unaofanywa kwa maksudi na baadhi ya watu ndani nan je ya
nchi kwa lengo la kutaka kuifanya Tanzania kama sio mahali sahihi pa
kuwekeza.
Biteko ameuambia ujumbe wa kampuni ya Ngwena kuwa, mabadiliko ya
sheria yamefanyika kwa kuzingatia maslahi ya pande zote mbili mwekezaji
na taifa kwa upande mwingine.
Amefafanua kuwa, tangu mabadiliko hayo yapitishwe hakuna malalamiko
ya kupingwa kwa marekebisho hayo kwakuwa yalizingatia maslahi mapana
ya kila upande na kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanakuwa rafiki na
ndio sababu mpaka sasa tangu marekebisho hayo yafanyike hakuna
kampuni au muwekezaji alie acha wala kuonyesha nia ya kufunga shuguli
zake kwa sababu ya marekebisho ya sheria.
Ameongeza kuwa, Tanzania inawahitaji sana wawekezaji na mara zote kila
panapokuwa na jambo haliendi sawa mara moja hukaa na kujadili na
mwekezaji na kutatua changamoto.
Ameitaka kampuni ya Ngwena kwenda kuwa mabalozi ili kuwaeleza
wengine kuhusu ukweli ulivyo kuhusu marekebisho ya sheria yaliyofanywa
na kuachana na upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu ambao
hawana dhamana ya kuyazungumzia masuala hayo.
Amewakaribisha watu na wawekezaji wote wanaotaka kupata ufafanuzi wa
jambo lolote kutembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Aidha, kwa upande wa kampuni ya Ngwena ukiongozwa na Meneja Mkuu
H.E Kavishe amemshukuru Waziri kwa ufafanuzi mzuri alioutoa na
kwamba walichokuwa wanakisikia na alichokisema waziri ni vitu tofauti na
kuongeza kuwa, kuonana kwao kumewafungua masikio na kupata ukweli
kutoka kwenye mtu sahihi na mwenye dhamana ya sekta ya madini.
Ameongeza kuwa, ni kweli upotoshaji waliokuwa wanaupata ungeweza
hata kuwarudisha nyuma, hivyo watakwenda kufikisha ujumbe kwa
wenzao.
Kikao hicho pia, kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof.
Simon Msanjila, Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mulabwa,
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria Edwin Igenge, na Mkurugenzi wa Sera
na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal, Kamishna masaidizi
anaeshuugulikia Migodi na Biashara Ali Ali na Kamishna masaidizi
anaeshugulikia Lesseni Maduh ….