Home Mchanganyiko HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE YASEMA ITAWEZA KUJIENDESHA KUPITIA MIRADI YAKE MIWILI...

HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE YASEMA ITAWEZA KUJIENDESHA KUPITIA MIRADI YAKE MIWILI YA SOKO NA STENDI ITAKAPO KAMILIKA

0

****************************************

Halmashauri ya mji wa Njombe imesema inatarajia kuanza kukusanya zaidi mil 500 kila mwaka katika miradi mikubwa ya Soko lenye hadhi ya kimataifa lililojengwa mjini humo pamoja na mradi wa kituo kipya cha mabasi miradi ambayo itagharimu zaidi ya bil 18 kwa ufadhili wa benki ya dunia .

Akizungumzia miradi hiyo mkurugenzi wa mji wa Njombe Illuminata Mwenda mara baada ya kufanya ukaguzi amesema katika mradi wa soko halmashauri itapata zaidi ya mil 300 kila mwaka huku kituo cha mabasi kikitajwa kuipa mapato ya zaidi ya mil 200 jambo ambalo litaipa uwezo halmashauri hiyo kujiendesha na kuwa mfano kwa wengine .

Pamoja na matarajio makubwa ya serikali katika miradi hiyo lakini kumekuwa na changamoto nyingi katika ujenzi wake ikiwemo changamoto ya kodi ya ongezeko la thamani VAT kwa mkandarasi wa mradi wa soko kuchelewa kukamilika jambo ambalo linamfanya Mhandisi Devid Tembo kutoa ombi kwa serikali kuu.

Mradi wa kituo kipya cha mabasi umefanikiwa kufika asilimia zaidi ya tisini hadi kukamilika kwake na tayari wakazi wa njombe wameanza kunufaika nao kama wanavyoeleza Paulina Agustino, Atu mwalongo mbao ni baba lishe na mama lishe wanasema wamepata fursa ya ajira zaidi

Mradi wa kituo cha mabasi tayari umeanza kazi huku wa soko ukitarajiwa kuanza mwezi wa kumi ambapo mradi wa soko umegharimu zaidi ya bil 9.3 huku kituo cha mabasi kikigharimu bil 9.6