kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire akionyesha kwa waandishi wa habari jana silaha aina ya SMG namba 260332 TZWD’KDU/IR/ 1990 mali ya KIDU inayodaiwa kuporwa kwa askari wa hifadhi ya Udzungwa Mwita Raphael (28) aliyeuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kabla ya kuporwa slaha hiyo na watu wanaodhaniwa na majangili
…………………..
Na Francis Godwin, Iringa
Jeshi la polisi linawashikilia watuhumiwa wanne kwa makosa mbali mbali likiwemo la kukutwa na meno ya tembo kamanda Bwire alisema kuwa katika tukio la kwanza lililotokea tarehe 1 june katika vijiji vya Mbawi ,Masisiwe , Chita na Ihimbo jeshi la polisi kwa kushirikiana na kikosi kazi cha taifa cha kupambana na ujangili ,kikosi cha kuzuia ujangili na TFS – Tanza nia Forest Service walifanya msako wa pamoja na kuwakamata watuhumiwa wawili pamoja na silaha aina ya SMG iliyoporwa na watuhumiwa hao wa ujangili .
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire amewaeleza leo waandishi wa habari ofisini kwake kuwa watuhumiwa hao wa ujangili ndio ambao wamehusika la mauaji ya askari wa hifadhi hya Udzungwa wilaya ya Kilolo Mwita Raphael (28) aliyeuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali /silaha kifuani na kumpora silaha aina ya SMG namba 260332 TZWD’KDU/IR/ 1990 mali ya KIDU ambayo imepatikana na watuhumiwa hao wawili .
Mbali ya tukio hilo alisema kuwa watu wengine wawili wakazi wa kijiji cha Wenda kata ya Tanangozi wilaya ya Iringa walikamatwa na jeshi la polisi kwa kushrikiana na afisa wanyamapori walimkamata Geofrey Kiswaga (35) mkulima akiwa na Nelson Kiduru (31) wakiwa na meno ya Tembo mamatu yenye uzito wa 8Kg ambayo thamani yake bado kufahamika waliyokuwa wameyahifadhi kwenye mfuko wa salfeti kwenye pikipiki namba Mc 116 BMZ aina ya Fekoni iliyokuwa ikiendeshwa na Kiduru wakitokea kijiji cha Nyamihumu Kidamali .
Kuwa watu hao walikuwa wakielekea kijiji cha wenda kufanya biashara ya meno hayo kwa wanunuzi ambao bado wanatafutwa na jeshi la polisi .
Wakati huo huo jeshi la polisi mkoa wa Iringa limewataka wakazi wa mkoa wa Iringa kuondoa hofu wakati wa sikukuu ya Idd kwani jeshi la polisi limejipanga kuhakiisha ulinzi na usalama unawekwa katika maeneo yote ya starehe na ibada kwa waumini wa dini ya Kiislam.
Kamanda Bwire alitoa onyo kwa madereva wa pikipiki na vyombo vya moto kuendesha kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuepuka kuendesha vyombo hivyo wakiwa wamelewa pombe huku akiwataka wananchi mkoani hapa kutoondoka wote majumbani kwao kwenda katika starehe kwani kufanya hivyo ni kukaribisha wezi nyumbani .
Aidha jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia Jupista Mhinza (30) mkazi wa kijiji cha Kilolo mkoani hapa kwa tuhuma za kumchoma na kijinga sehemu za siri mtoto wake wa miaka 6 baada ya kuchelewa kurudi nyumbani .
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Bwire aliwaeleza waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku katika kijiji cha Kilolo kata ya Kasanga tarafa ya Kasanga wilaya ya Mufindi ,ambapo mwanamke huyo alichukua uamuzi huo baada ya mtoto huyo ambae ni mwanafunzi wa shule ya msingi Kilolo kuchelewa kurudi nyumbani .
” mtoto huyo alikuwa akicheza na watoto wenzake hivyo kuchelewa kurudi nyumbani kitendo kilicho mkwaza mama mazazi na kuamua kuanza kumshambulia kwa kipigo na kisha kuamua kumchoma na kijinga cha moto katika sehemu zake za siri na kumjeruhi vibaya ” alisema kama Bwire
Mtoto huyo amelazwa katika kituo cha afya Kasanga akiendelea na matibabu na mwanamke huyo anashikiliwa na jeshi la polisi na atafikishwa mahakamani kwa tuhuma hiyo ya kumjeruhi mtoto huyo .