Waziri wa Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba akikagua mifuko mbadala inayotengenezwa na kiwanda cha Africa Paper bag kinachotengeneza mifuko hiyo leo katika zoezi la kutembelea viwanda ambavyo vinatengeneza mifuko hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Africa paper bag kilichopo Chang’ombe Jijini Dar es Salaam, ni moja ya mafanikio ambayo wameyapata hasa kupata ajira kupitia viwanda hivyo baada ya serikali kukataza mifuko ya plastiki
Baadhi ya wafanyakazi katika kiwanda cha utengenezaji mifuko mbadala Geen Earth Paper Product kilichopo Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam wakiwa wanatengeza mifuko mbadala kama ajira kwao
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanda cha Africa Paper Bag Bw.Hasnain Mauji akimueleza Waziri wa Muungano na Mazingira Mh.January Makmba namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi katika utengenezaji wa mifuko Mbadala
***************************************
Kuondoka kwa mifuko ya plastiki kumeibua fursa mpya,ajira ,mapato na kuinua uchumi shirikishi katika nchi hasa kutokana na viwanda vingi vimejitkeza katika kuzalisha mifuko mbadala kwa wingi pamoja na kuongeza wafanyakazi wazawa kwa wingi
Hayo yamesemwa na Waziri wa Muungano na Mazingira Mh. January Makamba katika zoezi la kutembelea viwanda mbalimbali vilivyopo jijini Dar es Salaam ambavyo vipo kwaajili ya kuzalisha mifuko mbadala.
Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam Mh. Makamba amesema kuwa serikali mpaka sasa imesajili wafanyabiashara na viwanda 80 nchi nzima ambao watakuwa wakizalisha mifuko mbadala kwa wingi.
“Mpaka sasa tunavitambua jumla ya viwanda 80 na wafanyabiashara nchi nzima tumekutana nao na kuwasajili katika orodha yetu ambao ni wazalishaji na waingizaji japo tunaamini wapo wengi ambao atujakutana nao hivyo wanaweza kuongezeka na kufikia 200”. Amesema Mh. Makamba.
Aidha Mh.Makamba amesema kuwa watu wengi walikuwa na wasiwasi kuhusiana na mifuko ya plastiki kutokuwepo kunaweza kusabisha kukosa ajira na mapato jambo ambalo si la kweli kutokuwepo kwake kumeibua uchumi mpya na shirikishi.
Kwa Upande wa Kaimu Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha mifuko Mbadala Afrika paper bag Limited Bw. Hasnain Mauji amesema kuwa kiwanda chao kimekuwa kikizalisha mifuko mbadala takribani mifuko laki 5 kwa siku ikiwa lengo lao kuzalisha mifuko hiyo Milioni 1 kwa siku hivyo kuna mashine kadhaa wameziagiza kwaajili ya uzalishaji.
“Ajira tumeongeza imekuwa mara mbili kulinganisha na mwanzo tulikuwa na watu 30 kwasasa tuna watu 60 na tunategemea zikija mashine nyingine tunaweza kuwa mpaka 100”. Amesema Bw. Mauji.
Hata hivyo kwa upande wa Mkurugenzi wa Kiwanda cha Green Earth Paper Product ambacho kinazalisha mifuko mbadala Bi. Angela Kessy amesema kuwa mwanzo kiwanda chao kilikuwa na changamoto kubwa na kutaka kukifunga ila baadae wakaamua kukiendeleza mpaka kufikia leo serikali kukataza mifuko ya plastiki na wao kuwatengenezea njia ya kupata masoko.
“Kiwanda chetu pia kinatoa fursa kushirikiana na watu wa SIDO kwaajili ya kutoa mafunzo ya utengenezaji mifuko hivyo basi nawaomba watanzania kupitia SIDO waweze kujitokeza kupatiwa mafunzo kwaajili ya utengenezaji wa mifuko hiyo”. Amesema Bi. Angela.