Waziri wa Muungano na Mazingira Mheshimiwa January Makamba akiongea na Mmoja wa Wafanyabiashara wadowadogo katika maendeo ya Kariakoo katika zoezi la Ukaguzi wa Mifuko ya Plastiki
Waziri wa Muungano na Mazingira Mh. Makamba akikagua moja ya Duka la kuuza Mifuko ya Jumla katika soko la Kariakoo Jijini Dar es Salaam Katika Zoezi la Ukaguzi wa Mifuko ya Plastiki katika Jiji Hilo.
**************************************
Serikali imewapongeza watanzania kulichukulia suala la katazo la mifuko ya plastiki kuwa ni la muhimu hivyo kulidhaniwa kuwa watanzania wengi wangechukuliwa hatua kutokana na baadhi ya watu wamekuwa wakiwashawishi wenzao kutolichukulia suala hilo maanani.
Ameyasema hayo Waziri wa Muungano na Mazingira Mh. January Makamba wakati wa zoezi la kukagua mifuko ya Plastiki katika baadhi ya maduka na masoko Kariakoo.
“Wananchi wamelipokea kwa makini suala hili hasa wale wamama wanaouza Mapapai wamesema mwanzo walikuwa wanawalazimu kununua mifuko kwa ajili ya kuwafungia mifuko leo hii matajili wanakuwa na mifuko yao kununua mapapai”. Amesema Mh. Makamba
Aidha Mh. Makamba amewataka watumishi wa NEMC kuendelea kufanya kazi pasispokuweka mapumziko ya jumamosi na Jumapili ili kuhakikisha zoezi hilo kwenda vizuri kama walivyopanga.
Pamoja na hayo Mh. Makamba amesema kuwa Mkoa ambao utafanya vizuri utapata zawadi pamoja na Mtaa utakao fanya vizuri katazo la mifuko ya plastiki watapata zawadi ya shilingi milioni 3.
“Tutaweka utaratibu wa motisha kwa wale ambao watatoa taalifa kwa watakaovunja sheria na kuwaweka nguvuni ili iwe fundisho kwa wengine na hivyo zoezi hilo kuwa endelevu”
Hata hivyo Mh. Makamba amesema kuwa kumekuwa changamoto katika mifuko mbadala hasa katika suala la upatikanaji,Bei, pamoja na ubora hasa kutokana na wananchi wanavyolalamika.
“Serikali ilipoamua, sasa tunapiga marufuku mifuko ya plastiki lakini kuna wale wazalishaji walijua ni mzaha,sasa kuna makontena inakuja ikiwa na mifuko ya mbadala hivyo nchi yetu itakuwa na mifuko Mbadala yakutosha na kuwezesha kushuka kwa bei ya mifuko hiyo”. Ameongeza Mh. Makamba.