Home Mchanganyiko SERIKALI NJOMBE YATAKA WAJASIRIAMALI KUBUNI MIFUKO MBADALA KWA KUTUMIA ZANA ASILIA

SERIKALI NJOMBE YATAKA WAJASIRIAMALI KUBUNI MIFUKO MBADALA KWA KUTUMIA ZANA ASILIA

0

*********************************

Ikiwa Tanzania imeanza kutekeleza agizo la kutumia mifuko mbadala ya Plastiki hii leo mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe Comrade Ally Kassinge ameendesha zoezi la kukusanya mifuko iliyopigwa marufuku na kutangaza mifuko mbadala iliyotengenezwa viwandani na wabunifu asilia.

Akizungumza mara baada ya kuendesha zoezi hilo la kukusanya mifuko iliyopigwa marufuku kwasababu ya madhara yake katika mazingira  katika kijiji cha Ilembula na Igwachanya mkuu huyo wa wilaya amewataka wabunifu na wajasiriamali kutumia katazo hilo kama fursa kwa kubuni mifuko mbadala wa plastiki kwa kutumia zana za asilia kwa kuunda vikapo.

“Muione mifuko ya plastiki kama bangi yeyote atakae kamatwa anacho”Kassinge alisema.

Akitoa ufafanuzi kuhusu adhabu zitakazotolewa kwa watakao bainika kuendelea kutumia mifuko iliyopigwa marufuku afisa mazingira wilaya ya Wanging’ombe Frank Ngogo anasema kutakuwa na adhabu kali ikiwemo ya fedha, kifungo jela na wkati mwingine vyote kwa pamoja.

Kwa Upande wao wananchi na baadhi ya wafanyabiashara wanasema katazo hilo limekuwa la ghafra kiutekelezaji lakini wanakubaliana nalo kwa kuwa lina nia njema

Katika zoezi hilo mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Ally Kassinge ametumia hadhara hiyo kutamburisha kampeni mpya wilayani kwake aliyoipa jina “Ana Kwa Ana na Kiongozi” yenye lengo la kukutana na mwananchi wa chini kabisa kusikiliza kero zao