Home Mchanganyiko DK.MABODI AFUNGUA MAFUNZO YA UWT MKOA WA MJINI.

DK.MABODI AFUNGUA MAFUNZO YA UWT MKOA WA MJINI.

0

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi akifungua Mafunzo ya Siku Moja ya UWT Mjini Unguja, kuanzia ngazi za Wadi hadi Mkoa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Sheikh  Idrissa Abdul Wakili uliopo Kikwajuni

BAADHI ya Viongozi na Watendaji wa UWT Ngazi za Wadi hadi Mkoa wa Mjini Unguja.

*****************************************

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

 WANAWAKE wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Tanzania Mkoa wa Mjini Unguja wametakiwa kujipanga vizuri kwa kuhakikisha CCM inapata Ushindi mkubwa wa Kihistoria katika Uchaguzi Mkuu wa Dola mwaka 2020.

Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi wakati akifungua Mafunzo Elekezi ya Kuwajengea Uwezo Viongozi mbali mbali wa UWT kuanzia ngazi za Wadi hadi Mkoa wa Mjini yaliyofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul Wakili Kikwajuni Unguja.

Dk.Mabodi amesema Wanawake wa CCM wanatakiwa kuwa Mstari wa mbele katika kuandaa Mazingira rafiki ya upatikanaji wa Ushindi wa Chama Cha Mapinduzi katika UchaguzI Mkuu ujao, kwa kuongeza Wanachama wapya na kuhakikisha wanaipigia kura nyingi CCM katika Uchaguzi Mkuu Ujaop.

Amesema  Wanawake wana historia kubwa na nzuri ya kufanikisha harakati za ushindi wa Chama na mikakati mbali mbali ya Ukombozi wa Nchi za Afrika.

Alieleza kwamba UWT pamoja na Jumuiza zingine za CCM zinatakiwa kushirikiana pamoja katika kuandaa mazingira ya Ushindi katika Uchaguzi ujao ili kutimiza kwa vitendo kauli mbiu ya Umoja ni Ushindi ndani na nje ya CCM.

Akizungumzia Mafunzo hayo Naibu Katibu Mkuu huyo Dk.Mabodi,amesema Mafunzo ni jambo muhimu sana katika shughuli za Kisiasa kwani Viongozi na Watendaji wanajengewa uwezo wa masuala mbali mbali ili watekeleze majukumu yao kwa uhakika.

“Mafunzo haya yasiishie katika Ngazi ya Wadi tu bali yashuke mpaka ngazi za Matawi hadi Mashina kwa lengo la kuhakikisha Jeshi letu linakuwa na uwezo mkubwa wa kufanikisha Ushindi wa CCM Mwaka 2020.”alisema Dk.Mabodi.

Katika maelezo yake Dk.Mabodi aliwasihi Wanawake hao kutojihusisha na masuala ya makundi ya kubeba Wagombe wa nafasi za Urais,Ubunge,Uwakilishi na Udiwani kabla ya Chama kutoa maelekezo ya kuana kampeni, na atakayebainika kufanya hivyo CCM itamchukulia hatua za Kimaadili.

Alisema CCM imekuwa Mstari wa mbele katika kuhamasisha Jamii kuenzi Amani na Utulivu Nchini ili kutoa nafasi pana kwa Serikali kutekelea kwa Ufasini shughuli mbali mbali za Maendeleo.

Alisema kwa kipindi cha miaka mitatu ya Uongozi wa Awamu ya Pili ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Nchi imepiga hatua kubwa za Kimaendeleo kutokana na kuimarika kwa Amani.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar  Ndugu Tunu Juma Kondo alisema Umoja huo unaendelea kutoa mafunzo mbali mbali ya kuwajengea uwezo Viongozi na Watendaji wake ili waingie katika harakati za Uchaguzi Mkuu ujao wakiwa na uwezo mzuri wa Kiutendaji na Kiuongozi.

Akitoa shukrani kupitia Magfunzo hayo  Mbunge wa Viti Maalum kupitia Mkoa wa Mjini Unguja Mhe.Asha Abdallah “Mshuwa”, alisema watayafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Mgeni rasmi kwa lengo la kuimarisha UWT na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla.

Amefafanua kwamba Wanawake wa Mkoa huo wapo tayari kupambana Vita ya Kisiasa na kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika ngazi mbali mbali katika Uchaguzi Mkuu Ujao.

Mafunzo hayo ya kuwajengea Uwezo wa masuala mbali mbali ya Kiuongozi Wanawake wa  UWT, yameandaliwa na  Wabunge na Wawakilishi wa Viti Maalum wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja.