*********************************
Akizungumza mara baada ya kuendesha zoezi hilo la kukusanya mifuko iliyopigwa marufuku kwasababu ya madhara yake katika mazingira katika kijiji cha Ilembula na Igwachanya mkuu huyo wa wilaya amewataka wabunifu na wajasiriamali kutumia katazo hilo kama fursa kwa kubuni mifuko mbadala wa plastiki kwa kutumia zana za asilia kwa kuunda vikapo.
“Muione mifuko ya plastiki kama bangi yeyote atakae kamatwa anacho”Kassinge alisema.
Kwa Upande wao wananchi na baadhi ya wafanyabiashara wanasema katazo hilo limekuwa la ghafra kiutekelezaji lakini wanakubaliana nalo kwa kuwa lina nia njema
Katika zoezi hilo mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe Ally Kassinge ametumia hadhara hiyo kutamburisha kampeni mpya wilayani kwake aliyoipa jina “Ana Kwa Ana na Kiongozi” yenye lengo la kukutana na mwananchi wa chini kabisa kusikiliza kero zao