MTOTO MMOJA AITWAYE MARIAM KANIZIO, MSUKUMA, MIAKA 12 MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI KIGONGO FERRY, ALIUWAWA KWA KUCHINJWA/KUKATWA SHINGONI NA KITU CHENYE NCHA KALI NA MWANAUME AITWAYE MADINDA MBOGO, MIAKA 32, MSUKUMA, MVUVI NA MKAZI WA KIGONGO FERRY, AMBAYE NI MPENZI/HAWALA WA MAMA WA MTOTO HUYO, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA, HUKO KIGONGO FERRY WILAYA YA MISUNGWI.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 28.05.2019 MAJIRA YA 03:00HRS USIKU, HII NI BAADA YA MGOGORO WA WIVU WA KIMAPENZI KATI YA MAMA WA MTOTO AITWAYE MAGENI MASHIMBA, MIAKA 50 NA MTUHUMIWA, NDIPO MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU ALIAMUA KUMUUA MTOTO HUYO AKIWA AMELALA KWA KUMCHINJA SHINGONI NA KITU CHENYE NCHA KALI (KISU). BAADA YA KUTENDA TUKIO HILO MTUHUMIWA ALIJARIBU KUJIUA KWA KUJIJERUHI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE IKIWA NI PAMOJA NA TUMBONI KWA KUJICHOMA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA BAADAE ALIKUNYWA SUMU AMBAYO HAIKUWEZA KUBAINIKA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LILIPATA TAARIFA JUU YA TUKIO HILO NDIPO LILIFANYA UFUATILIAJI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA HUYO NA WAKATI AKIPELEKWA HOSPITALI ALIFARIKI DUNIA. MIILI YA MAREHEMU WOTE WAWILI IMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA NDUGU WA MAREHEMU KWA TARATIBU ZA MAZISHI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA ONYO KWA BAADHI YA WANANCHI WENYE TABIA YA KUTENDA VITENDO VYA UKATILI KWA WATOTO AU WATU WENGINE KUWA WAACHE KWANI NI KINYUME NA SHERIA NA ENDAPO MTU/WATU WATABAINIKA HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO. SAMBAMBA NA HILO JESHI LA POLISI LINAOMBA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LAO, KWA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU NA WAHALIFU ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA;
Muliro J. MULIRO-ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.
29 MAY, 2019.