Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Wiliam Mwegoha,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kujionea hali halisi ya utekelezaji wa katazo Mifuko ya Plastiki katika Soko la Majengo jijini Dodoma.
Afisa Mazingira wa Halmashauri ya jiji la Dodoma ambaye pia ni Mjumbe wa kikosi kazi hicho Bwana Ally Mfinanga,akitolea ufafanuzi mara baada ya kufanya ziara ya kujionea hali halisi ya utekelezaji wa katazo Mifuko ya Plastiki katika Soko la Majengo jijini Dodoma
Baadhi ya viongozi kutoka NEMC wakiwa na Afisa Mazingira wa Halmashauri ya jiji la Dodoma ambaye pia ni Mjumbe wa kikosi kazi hicho Bwana Ally Mfinanga,wakiangalia mifuko itakayotumika baada ya Serikali kupiga maarufuku Mifuko ya Plastiki mara baada ya ziara ya kujionea hali halisi ya utekelezaji wa katazo Mifuko ya Plastiki katika Soko la Majengo jijini Dodoma
Afisa Mazingira wa Halmashauri ya jiji la Dodoma ambaye pia ni Mjumbe wa kikosi kazi hicho Bwana Ally Mfinanga,akimuelezea jambo mwananchi kuhusu katazo la Mifuko ya Plastiki mara baada ya kufanya ziara ya kujionea hali halisi ya utekelezaji wa katazo Mifuko ya Plastiki katika Soko la Majengo jijini Dodoma.
Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
…………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kwa kushirikiana na Baraza la mazingira ,kikosi kazi cha katazo la mifuko ya plastiki ,wenzao kutoka jiji pamoja na ofisi ya Mkuu wa mkoa wamefanya ziara katika soko kuu la majengo na maeneo mengine kwa ajili ya kujionea hali halisi juu ya katazo la mifuko ya plastiki na kuangalia utayari wa wananchi katika kuhakikisha kwamba wanatekeleza agizo la serikali .
Akizungumza katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Idara ya mazingira ofisi ya makamu wa Rais Profesa wiliam Mwegoha amesema kuwa serikali imezimia kusitisha juu ya matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia tarehe moja 1 ya mwezi wa sita hivyo kumekuwa na ueleimishaji wa jamii kwa kiasi kikubwa.
”Nawaomba wananchi,wafanyabiashara wauzaji na watumiaji kutii sheria ifika kesho na wajisarimie wenyewe kama mlivyoona kwenye ofisi ya mtendaji tayari watu weshaipeleka mifuko hiyo”amesema Prof.Mwegoba
Aidha, ameongeza kuwa elimu iliyokuwa ikitolewa imeenda vya kutosha kwani wamepita katika maeneo mbalimbali na wamekuta wananchi wana uelewa juu ya katazo hilo na wapo tayari kusalimisha.
Kwa upande wake Afisa mazingira wa halmashauri ya jiji la Dodoma lakini pia ni mjumbe wa kikosi kazi hicho Bwana Ally Mfinanga amesema kwa niaba ya mkurugenzi wa jiji la Dodoma wameendelea kutekeleza agizo la serikali kutoa elimu kuhusiana na katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki.
Sambamba na hilo amesema wanawaelimisha wananchi kuacha na matumizi ya mifuko ya plastiki na kutumia mifuko mbadala ili kuweka mazingira safi.
“ Tumeitikia kwa vitendo agizo la Waziri mkuu la kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki, na sisi kama unavyoona leo hii tumefanya ziara katika soko hili la Majengo kwa kutoa hamasa kwa wananchi kuacha na matumizi ya mifuko ya Rambo ambayo inamadhara makubwa katika ustawi wa mazingira”amesema Mfinanga
Nao baadhi ya wafanyabishara wamesema kuwa mbali na yakuwa mifuko ya mbadala ipo lakini kuna changamoto ya ununuzi wa mifuko hiyo kwani imekuwa ni ya bei ghali , hivyo wameiomba serikali kuleta hata ya bei ndogo ila kila mtu wa chini aweze kupata .
”Sisi tunaiunga mkono Serikali la kupiga marufuku wa mifuko ya Ramba Rai yetu kwa Serikali tunaomba mifuko mbadala zipunguzwe bei ili ziendane na kipato chetu wamesema”
Ikumbukwe kuwa katazo la mifuko ya plastiki ilitolewa Bungeni Jijini Dodoma na waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kasim Majaliwa siku ya jumanne April 9,2019 kwenye mkutano wa 15 wakati akihitimisha hoja ya Bajeti ya ofisi ya waziri mkuu ,taasisi zake na mfuko wa Bunge kwa mwaka 2019/2020 ambapo alisema kuwa kuanzia juni mosi,2019 itakuwa ni marufuku kutengeneza,kuingiza,kuuza na kutumia mifuko ya plastiki kwaajili kubebea bidhaa na matumizi yake yatakoma ifikapo mei 31,2019.