Kada wa CCM na Mwanachama Philipo Mwakibinga niliyetokea upinzani na kujiunga na chama hicho amesema ipo tofauti kubwa kati ya Chama cha mapinduzi CCM na vyama vingine wa siasa hapa nchini.
Mwakibinga ameyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari Magomeni jijini Dar es salaam leo wakati akijibu hoja za aliyekuwa mwanachama wa CCM kabla ya kurudi upinzani Bw. Gango Kidera ambaye aliyerejea CHADEMA hivi karibun.
Mwakibinga amesema CCM ni chama chenye kuongozwa na, Kanuni, taratibu na miongozo. Hili halipo katika chama chochote cha Upinzani. Huko kwa wenzetu ambako siye tumekulia Kanuni, taratibu na miongozo vipo kwenye nguvu za mtu mmoja tu.
Mwakibinga ametolea Mfano Chama cha CHADEMA akisema kila jambo lipo katika hatima ya mikono ya Kiongozi mmoja. Hivyo mtu anapotoka CCM nakurudi huko jua kashindwa kuishi kwa kanuni, taratibu na miongozo bali anapenda kuishi bila utaratibu.
Ameongeza kwamba huwezi kujiunga CCM kwa lengo la kwenda kupata cheo CCM ni chama kilichojipambanua kwa kanuni zake, na taratibu za kila jambo ziko kwenye maandishi, Hivyo kutaka vyeo bila kufuata utaratibu Hii si sawa
“Ndani ya CCM upatikanaji wa uongozi kwa nafasi za kugombea ni kila baada ya miaka mitano. Hivyo kama uchaguzi umefanyika na hukupata nafasi inabidi uunge mkono waliochaguliwa kwa ajili ya kufanya kazi ya Chama na Taifa kwa ujamla hii ndiyo demokrasia yenye misingi ya haki na usawa ameongeza” Philip Mwakibinga.
Ameongeza kwamba nafasi za kuteuliwa hizi hupatikana kulingana na matakwa ya kanuni, taratibu na mahitaji ya mamlaka za uteuzi kwa mujibu wa miongozo. Hivyo waliokosa nafasi kama Bw. Gango Kidera bado wanahitaji kupata nafasi za kugombea lazima usubiri baada ya kipindi hicho kupita.
Ameongeza kwamba Gango Kidera ametoka CHADEMA anataka uchaguzi ufanyike ili kupata madaraka kwa sababu tu kahamia. Hakuna demokrasia ya namna hiyo CCM labda huko CHADEMA ndiko utayakuta hayo.
Mwakibinga ameleza kuwa Kidera alipaswa kufanya utafiti kwanza juu ya CCM kabla hajahamia na kushindwa kufanya hivyo ni wazi kajianika kuwa mtu asiye makini na hii ni dalili mbaya kwa wanasiasa wa aina yake. maana hawana mapenzi ya kweli na Demokrasia bali wanakua wanaajenda binafsi tofauti na malengo madhubuti ya chama cha siasa.
“Chama cha Mapinduzi CCM ni chama bora zaidi barani Afrika. Ndicho chama cha ukombozi kinachotoa dira ya maendeleo. Mtakumbuka Prof. Lumumba wa Kenya alitaja vyama viwili tu vinavyostahili kubaki barani Afrika katika vyama hivi CCM ni kimojawapo” Ameongeza.
Amesema kutokana na mfumo bora wa CCM ndiyo maana chama hiki kimetoa Rais Bora barani Afrika Ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM huyu si mwingine ni Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
“Ninyi ni mashahidi mmeona namna anavyopokelewa na kuhitajika kwenye mataifa ya wenzetu. Tumeona Alipokwenda Afrika Kusini , Namibia na Zimbabwe. Mapokezi aliyoyapata na namna anavyoheshimika . Hii ni alama kubwa na tunu kwa Taifa letu.