***********************************
Klabu ya Inter Milan inayoshiriki ligi kuu ya Italia maalufu Seria A imemtangaza aliyekuwa kocha wa Chelsea Antonio Conte kuwa kocha wao mpya muda mfupi baada ya kumtimua aliyekuwa kocha wa timu hiyo Luciano Spalletti.
Spalletti licha ya kuiongoza klabu hiyo na kuipeleka kushiriki ligi ya Mabingwa Ulaya lakini haijasaidia kuwashawishi viongozi wa klabu hiyo kuendelea naye.
Conte ambaye alitimuliwa na klabu ya Chelsea hakuweza kupata timu nyingine kwa msimu mmoja hivyo kwasasa katika msimu ujao ataitumikia klabu hiyo yenye masikani yake mjini Milani.