Home Mchanganyiko CWT YATOA UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA JUU YAKE

CWT YATOA UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA JUU YAKE

0

RAIS wa chama cha walimu nchini (CWT) Bi.Leah Ulaya,akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma kuhusu tuhuma za habari zilizochapishwa kwenye moja ya gazeti la kila wiki nchini kulia Kwake ni Katibu Mkuu wa chama hicho Deus Seif.

Sehemu ya baadhi ya viongozi na wanachama wa  chama cha walimu nchini (CWT) wakifuatilia ufafanuzi kutoka kwa Rais wa chama hicho Bi.Leah Ulaya,) leo jijini Dodoma kuhusu tuhuma za habari zilizochapishwa kwenye moja ya gazeti la kila wiki nchini

RAIS wa chama cha walimu nchini (CWT) Bi.Leah Ulaya,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma kuhusu tuhuma za habari zilizochapishwa kwenye moja ya gazeti la kila wiki nchini kulia Kwake ni Katibu Mkuu wa chama hicho Deus Seif.

Katibu Mkuu wa chama hicho Deus Seif,akitolea uafafanuzi Hoja iliyoandikwa na gazeti moja  ya kudai kuwa fedha za chama alitumia kwenda kuangalia mechi ya Cape Verde na Taifa Stars , pamoja na hoja ya kuajiri watu wenye vyeti feki.

Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

…………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Chama cha walimu nchini (CWT) kimetoa ufafanuzi kuhusu habari zilizochapishwa kwenye moja ya gazeti la kila wiki nchini zilizo kituhumu chama hicho kwa ufisadi na upendeleo na kudai kuwa siyo za kweli.

Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa chama hicho Bi.Leah Ulaya,amesema kuwa wamesikitika na  kitendo cha gazeti hilo kuchapisha habari ambazo zinalengo la kukichafua chama hicho

Bi.Ulaya amesema kuwa  chama hicho kimelitaka gazeti hilo kuomba radhi vinginevyo watachukua hatua za kisheria.

Amesema kuwa habari hiyo lilikuwa na lengo la  kutufedheesha na kutuchafua chama cha walimu Tanzania, uongozi wa chama cha walimu na siyo hivyo tu bali walimu wote nchini kwa kuonekana kuwepo na ufisadi na upendeleo katika chama chetu kitu ambacho si kweli.

“Na mpaka sasa hatujui lengo la mwandishi na gazeti kwa ujumla ilikuwa nini?kutuchafua au kuuza gazeti kupitia idadi kubwa ya wanachama wetu”amehoji

Aidha Bi.Ulaya amezitaja hoja zilizoandikwa katika gazeti hilo ikiwa ni pamoja ile ya kudai kuwa vigogo wa kukipeleka chama katika mstari mwekundu.

Hoja nyingine ni ile ya chama hicho kufanya upendeleo katika ajira na kukiuka kanuni za ajira za chama pamoja na  kudai kuwa fedha za chama kutumika kwenda kuangalia mechi ya Cape Verde na Taifa Stars ambazo zilitumiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Deus Seif, ikiwa pamoja na hoja ya kuajiri watu wenye vyeti feki.

Akitolewa ufafanuzi juu ya matumizi ya fedha za chama hicho kwajili ya kwenda kuangalia mechi kati ya Cape Verde na Taifa stas katibu Mkuu Deus Seif, amesema kuwa yeye pia ni kiongozi wa chama cha mpira ngazi ya mkoa wa Geita hivyo alikwenda kama kiongozi wa chama cha mpira na si CWT.

Bw.Seifu amesema kuwa anashangaa  hoja ya kuajiri watu wenye vyeti feki kama amabvyo gazeti hili limeandika siyo kweli kwani mchakato wote ulifanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi.