Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto), akibadilishana hati za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa miaka mitano na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay, makubaliano yatakayoiwezesha NBC kusaidia mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo biashara nchini. NBC pia ilipokea mfano wa hundi ya Dola 1,000,000 kutoka PASS zitakazotumika kama dhamana katika mikopo ya kilimo itakayotolewa na benki hiyo. Hafla ilifanyika jijini Arusha leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Ofisa Mtendaji Mkuu wa PASS, Anna Shenalingigwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto), akisaini hati za makubaliano ya ushirikiano wa miaka mitano na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay, makabaliano yatakayoiwezesha NBC kusaidia mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo biashara nchini. NBC pia ilipokea mfano wa hundi ya Dola 1,000,000 kutoka PASS zitakazotumika kama dhamana katika mikopo ya kilimo itakayotolewa na benki hiyo. Hafla ilifanyika jijini Arusha leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Ofisa Mtendaji Mkuu wa PASS, Anna Shenalingigwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto), akipokea mfano wa hundi wa Dola 1,000,000 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay makabaliano yatakayoiwezesha NBC kusaidia mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo biashara nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Ofisa Mtendaji Mkuu wa PASS, Anna Shenalingigwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto, walioketi) na Mkurugemzi Mtendaji wa PASS, Nicomed Bohay (kushoto kwake), wakipozi kwa picha ya kumbukumbu pamoja na watumishi wa taasisi hizo mbili mara baada ya kumalizika kwa tuki hiyo mjini Arusha leo.