Mwakilishi na Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw.Tirso Dos Santos,amevitaka vyombo vya habari nchini kuendelea kuandika habari zenye kuelimisha jamii ili kuondoa dhana ya unyanyasaji wa kijinsia.
Hayo ameyasema jana jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa waandaji wa vipindi vya Radio nchini nzima.
Bw.Santos amesema kuwa vyombo vya habari vinawajibu mkubwa kwa jamii na kuendelea kutoa elimu kwa kupitia radio au magazeti ili kukomesha ama kuondoa kabisa suala la unyanyasaji wa kijinsia.
“Kila siku jamii wanapata habari kupitia vyombo vyenu hivyo mkiandaa vipindi vyenye kueleimisha jamii itasaidia kukomesha suala la unyanyasaji wa kijinsi kwa makundi mengi”amesema Santos.
Aidha Bw.Santos alisema kuwa mimba za utotoni zimekuwa changamoto kutokana na vijana kuingia kuanzia umri wa miaka 14 mpaka 19 kujiingiza kwenye mahusiano yaliyosababisha mimba hizo.
Amebainisha kuwa changamoto hizo zimesababisha wanafunzi wengi kushindwa kutimiza ndoto zao za elimu hasa watoto wa kike kutokana na kuingia kutunza familia.
Hata hivyo aameishukuru Serikali kupitia wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa ushirikiano wao uliowesha kufanikiwa katika kampeni hizo.
Naye Naibu Katibu Mtendaji Utawala na Fedha wa shirika la Unesco hapa Nchini Fransis Msungu, amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza na kujenga uelewa zaidi kwa washiriki.
Msungu amesema kuwa Taifa hili linahitaji waandishi wa habari watunzi wa vitabu pamoja na wabunifu wenye maono ya kuandaa habari ili kuchochea maendeleo na ustawi kwenye jamii yetu.
Hivyo amesema kuwa wanahabari hapa nchini wanamchango mkubwa katika kuchangia na kutetea amani ya maeneo wanapoishi na Taifa kwa ujumla .
Alisisitiza kuwa Unesco wameendelea kutoa mafunzo hayo kupitia makundi mbalimabli wakiwemo wandishi ili kufikisha elimu ya afya ya uzazi salama,ukimwi pamoja na kuzuia ukatili wa kijinsia.