NA MWAMVUA MWINYI,KISARAWE
MAHAKAMA ya wilaya ya Kisarawe,mkoani Pwani imejinasua kwenye kesi ya katibu wa kamati ya wakulima wa kijiji cha Chanika Jackson Rwehumbiza pamoja na wizara ya maliasili na utalii na kushauri ipelekwe kwenye mabaraza ya ardhi.
Kesi hiyo namba 24 ya mwaka 2018 ya mgogoro wa ardhi, ilisomwa mbele ya hakimu Devotha Kisoka na mwendesha mashtaka Joseph Mwaipaja ambapo alieleza, Rwehumbiza alishtakiwa kwa kosa la kuingia katika hifadhi ya Kazimzumbwi bila kibali.
Kesi imesikilizwa pande zote na mahakama imegundua kwamba eneo hilo lina mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na maliasili.
Kwa mujibu wa sheria mahakama ya jinai inapogundua chanzo ni mgogoro wa ardhi inashauri kesi hiyo ipelekwe kwenye mabaraza ya ardhi,”::Kwa maana hiyo,imegundua ni mgogoro wa ardhi hivyo shauri hilo liende kwenye mamlaka ya ardhi ili kama likirudi lirudi kama jinai.
Alielezea kwamba,tafsiri yake mahakama haijatamka eneo ni la nani baina ya pande hizo mbili na haiwezi kutamka mmiliki halali wala mshindi ni nani wa kesi kwakuwa si mahakama husika wa usuluhishi wa migogoro ya ardhi.
Kwa upande wake, Rwehumbiza alishukuru maamuzi hayo na kudai hukumu imetenda haki .
Alisema mgogoro huo ni wa miaka 18 na wao hawana nia ya kupingana na serikali hivyo wanaomba mipaka iwekwe ili kujua wananchi wanapaswa kuishia wapi.
Rwehumbiza alibainisha,hukumu hiyo ni ya tano tangu kuanza kushtakiwa na zote hazijakatwa rufaa ameiomba serikali ya awamu ya tano pamoja na chama cha mapinduzi (CCM) kuwasaidia kuingilia kati mgogoro huo ili waishi kwa amani.
“Sisi tunarudi mashambani kuanzia leo,tumepata hasara na kuishi bila kuendelea na shughuli zetu kipindi kirefu,”Tumelilia haki yetu miaka sasa na hatimae leo mungu katusaidia”alifafanua.
Mkulima mwingine Mohammed Sutty alisema wapo wananchi zaidi ya 1,000 katika sakata hilo ,haki imechelewa lakini hatimae wameipata