Bodi ya nyama hapa nchini imewataka wamiliki wa mabucha, wauzaji wa nyama kuhakikisha kuwa wanaboresha na kuim arisha mabucha yao na biashara zao kabla ya september 30 ambapo bodi hiyo itaanza msako mkali ikiwa ni pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya usalama kwa ajili ya kulinda afya ya mlaji
Hayo yameelezwa na kaimu msajili wa bodi hiyo bw Imani Sichalwe wakati akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kutoa elimu ambayo ilienda sambasamba na ufungaji wa mabucha ambayo hayana vigezo kwa mkoa wa Arusha
Sichalwe alisema kuwa wamiliki na wauzaji wa nyama wanatakiwa kutambua kuwa ifikapo september 30 kama watakuwa hawajakidhi viwango vyote vya uuzaji wa nyama basi watachukuliwa sheria kali
alisema vigezo ambavyo wanatakiwa kukamilisha kwa sasa ni pamoja na ujenzi bora wa mabucha, uvaaji wa sare ambazo zinatakiwa kisheria kama vile kofia nyeupe,mabuti meupe, heproni ngumu nyeupe, makoti meupe, upimaji wa afya zao mara kwa mara(Kila baada ya miezi sita)
Pia alisema mbali na hayo mabucha yanatakiwa kuwa na mashine maalumu kwa ajili ya kukatia nyama ambapo kwa sasa bado yapo baadhi ya mabucha ambayo yanatumia magogo kukatia nyama jambo ambalo ni hatari hata kwa afya ya mlaji
Alidai kuwa muuzaji wa nyama anapotumia gogo kukatia nyama kuna madhara mbalimbali yakiwemo madhara ya kiafya,m lakini hata kwake kuna madhara pia kwa kuwa nyama nyingi inaweza kupotea
kutokana na hayo alidai kuwa bado bodi hiyo imetoa muda maalumu wa kuhakikisha kuwa kila bucha la nyama linakuwa kwenye viwango vinavyotakiwa lakini kama watapuuza suala hilo basi hatua kali zitachukuliwa kwa ajili ya kulinda afya ya mlaji