Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, akizungumza wakati wa kikao cha pamoja kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kilichojadili utekelezaji wa Programu ya Usimamizi wa Fedha za Umma-Awamu ya Tano (PFMRP-V), kushoto ni Bi. Trine Lunde Mwenyekiti mwenza wa kundi la Washirika la Maendeleo wanaofadhili mradi huo, kikao hicho kimefanyika Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamisi Shaaban akizungumza jambo wakati wa kikao na Washirika wa Maendeleo (hawapo pichani), wanaofadhili mradi wa Programu ya Usimamizi wa Fedha za Umma kwenye ukumbi wa Wizara Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (kushoto) akiongoza kikao cha pamoja kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleokilichojadili utekelezaji wa Programu ya Usimamizi wa Fedha za Umma-Awamu ya Tano (PFMRP-V), kulia ni Bi. Trine Lunde Mwenyekiti mwenza wa kundi la Washirika la Maendeleo wanaofadhili mradi huo, kikao hicho kimefanyika Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kikao cha pamoja kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kilichojadili utekelezaji wa Programu ya Usimamizi wa Fedha za Umma-Awamu ya Tano (PFMRP-V), ijini Dodoma.
Wadau wakifuatilia kikao cha Washirika wa Maendeleo wanaofadhili Programu ya Usimamizi wa Fedha za Umma, kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (hayupo pichani), Jiijni Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Richard Mkumbo (kulia), akifafanua jambo kwenye kikao cha pamoja kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kilichojadili utekelezaji wa Programu ya Usimamizi wa Fedha za Umma-Awamu ya Tano (PFMRP-V, kikao hicho kimefanyika Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamisi Shaaban wa kwanza kulia, Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Tixon Nzunda (katikati), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Richard Mkumbo wakati wa kikao Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali baada ya kuhitimishwa kwa kikao cha pamoja kati ya Serikali na Wadau wa Maendeleo kilichojadili utekelezaji wa Programu ya Usimamizi wa Fedha za Umma-Awamu ya Tano (PFMRP-V).
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
…………………….
Na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James amewashukuru Wadau wa Maendeleo kwa kuisaidia Serikali kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha za umma iliyosaidia kuongeza tija katika ukuaji wa uchumi wa nchi na utoaji huduma bora kwa wananchi
Bw. James ametoa shukrani hizo Jijini Dodoma wakati wa kikao cha mwisho kwa mwaka wa fedha 2018/2019 cha Wadau wa Maendeleo na Serikali kilichojadili maendeleo ya utekelezaji wa Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano (PFMRP-V) ambao utekelezaji wake umeingia mwaka wa pili na unaotarajiwa kukamilika mwaka wa fedha 2021/2022
Programu ya Maboresho na Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano, utagharimu shilingi bilioni 152.3 katika kipindi cha miaka mitano kuanzia Julai mwaka 2017 hadi Juni, 2022, ambapo unatarajia kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kudhibiti mianya yote ya matumizi mabaya ya fedha za Serikali.
Alisema kuwa katika kipindi cha miaka miwili cha utekelezaji wake, umeonesha mafanikio makubwa ikiwemo usimikaji wa mifumo zaidi ya 7 ya kieletroniki ya kukusanya na kudhibiti mapato ya Serikali.
” Mifumo hii ukiwemo mfumo wa GePG umesaidia sana kuongeza ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali pamoja na kodi, imeongeza udhibiti wa matumizi, misamaha ya kodi na kusaidia upelekaji wa rasilimali fedha kwenye miradi ya kipaumbele ya kitaifa na hatimaye kusaidia usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo” alisema Bw. James
“Wizara ya Fedha na Mipango imejipanga kuendeleza kazi nzuri za programu ili kuendelea kuunga mkono agenda ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli; katika kusimika mifumo na maboresho ya uhakika katika kusimamia fedha za umma. Hatua hii itachochea maendeleo ya kiuchumi yanayowagusa watanzania wote”
Kwa upande wake, Mwenyekiti mwenza wa kundi la Washirika wa Maendeleo wanaofadhii Program ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Tano (PFMRP-V), Bi. Trine Lunde, alielezea kuridhishwa kwao na namna Tanzania inavyotekeleza na kusimamia programu hiyo ambayo amesema imeleta tija katika usimamizi wa fedha za umma nchini.