Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mnara wa Tigo ulipandishwa hadhi kutoka 3G kwenda 4G wilayani Mpanda jana. Kushoto ni Meneja Mauzo ya Kanda ya Kusini kutoka Tigo, Francis Ndada.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga (kushoto) akitembelea banda la mauzo ya bidhaa za mawasiliano kama simu muda mfupi kabla ya kuzindua mnara wa Tigo ulliopandishwa hadhi kutoka 3G kwenda 4G. Kulia ni Meneja Mauzo ya Kanda ya Kusini kutoka Tigo, Francis Ndada
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga akizungumza na wananchi wa wilaya ya Mpanda (hawapo pichani) muda mfupi kabla ya kuzindua mnara wa Tigo ulipandishwa hadhi kutoka 3G kwenda 4G wilayani Mpanda jana. Kulia ni Meneja Mauzo ya Kanda ya Kusini kutoka Tigo, Francis Ndada na wa kwanza kulia na Oliver Baltazar na Laverty Khana ambao ni wafanyakazi wa Tigo
Meneja Mauzo ya Kanda ya Kusini kutoka Tigo, Francis Ndada (kushoto) akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga (kati kati) muda mfupi baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuzindua mnara wa Tigo uliopandishwa hadhi kutoka 3G kwenda 4G wilayani Mpanda jana.
……………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
Mji wa Mpanda, Katavi sasa umeunganishwa kwenye mtandao wa 4G baada ya kampuni ya Tigo kuzindua mnara wenye uwezo wa kutoa huduma hiyo ya mtandao wenye kasi.
Huduma hiyo mpya,itawezesha wateja wa Tigo wilayani Mpanda kunufaika na huduma bora za kupiga simu, intaneti, kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao huo.
Akizindua mnara huo mjini, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga, aliipongeza Tigo na uongozi wake kwa mafanikio ya kuleta mnara huo wa kisasa, ambao utakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa wilaya hiyo.
“Kwa niaba ya watu wa Mpanda, napenda kuwashukuru sana Tigo kwa kazi nzuri. Hakika, huu mnara ambao tunaouzindua leo utachochea kwa kasi kubwa shughuli zetu za biashara, utalii na kilimo tunazofanya hapa Mpanda,” alisema Matinga.
Meneja Mauzo ya Kanda ya Kusini kutoka Tigo, Francis Ndada, alisema kuongeza ufanisi wa mnara huo kutoka mtandao wa 3G kwenda 4G kuna maana kwamba wateja wa Tigo Mpanda wataweza kupata huduma zao kwa uharaka na urahisi zaidi.
“Kipaumbele chetu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma za teknolojia za kisasa kama mtandao wa 4G. Pia ni muhimu kutambua kwamba, teknolojia ya 4G imeongeza idadi kubwa ya watu kuunganishwa na intanet kupitia simu, na pia imezifungulia jamii zilizopo vijijini kuweza kupata huduma za kielektroniki katika nyanja za kibiashara, afya, elimu na serikali ambazo walishindwa kupata huko nyuma. Hivyo, kubadilisha kabisa namna watu watakavyojifunza na kufanya biashara,” alisema Ndada.
Uzinduzi wa mnara huu unaenda sambamba na ofa maalum kwa wateja wa Mpanda, ambapo wateja ambao watahudumiwa katika eneo ya mnara huo wa 4G, watazawadiwa GB 4 za intanet bure pale wanapobadilisha laini zao za simu na kuchukua za 4G. Wateja wataweza kutumia kifurushi hicho kwa muda wa siku 7.
Ndada pia alizungumzia kuhusu kazi ambayo Tigo inafanya kuwezesha sera ya TEHAMA ya Taifa na kuunga jitihada za serikali katika kujenga viwanda kwa kupanua na kuboresha wigo wa mtandao ili kuwezesha nchi kufaidika katika nyanja mbali mbali za kijamii kama uchumi na elimu kupitia mfumo wa kidijitali.
Mnara wa Mpanda ni wa tatu kuzinduliwa baada ya Kilolo, Iringa na Bariadi, Simiyu. Jumla ya minara 52 itazinduliwa katika kampeni hii ya nchi nzima kutoka kanda ya Ziwa, Kaskazini, Pwani na Kusini.
Minara mengine ambayo imeboreshwa na zitazinduliwa hivi karibuni katika Kanda ya Kusini ni Sumbawanga, Rukwa.